NA ABDI SULEIMAN.
JAMII imetakiwa kufahamu kuwa suala la uhifadhi wa maeneo ya bahari kwa sasa ni jambo ambalo haliepukiki, hii imetokena na kuwepo kwa vichocheo vingi vinavyochochea bahari kuhifadhiwa.
Moja cha ya vichocheo hivyo ni mabadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa idadi ya watu na kupungua kwa rasilimali za bahari siku hadi siku.
Haya yamelezwa na Mkuu wa PECCA Pemba Omar Juma Suleiman, wakati alipokua akizungumza na timu ya waandishi wa habari, katika ziara maalumu iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET), chini ya mradi wa Tuhifadhi Maliasili Tanzania, kutoka shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID).
Alisema kazi ya uhifadhi wa rasilimali hiyo, sio kazi ya serikali peke yake, bali ni kazi inayohitaji utayari wa jamii ili kushirikisha na serikali katika kuendeleza kutunza na kuhifadhi rasilimali za bahari ambazo ndio lulu kwa sasa.
“Isije ikafika siku ndugu zetu, watoto wetu na wajuku zetu wanakuja kujisikia vibaya, baada ya kusikia samaki na matumbawe yote yameharibiwa na wazazi wao, halitokuwa jambo zuri na lakuvutia,”alisema.
Alifahamisha kwa, ili kufikia malengo lazima jamii iwe tayari katika kuhifadhi rasilimali kwa vizazi endelevu, ikizingatiwa mabadiliko ya tabia nchi, ongezeko la watu, linapelekea rasilimali hiyo kutiwa kwa kiasi kikubwa.
Aidha alisema kuwa PECCA inawajibu wa kusimamimia rasilimali zote zilizomo katika bahari, kwa mujibu wa sheria ya uvuvi namba 7/2010 na pecca oda.
Akizungumzia nafasi ya wanawake na vijana katika uhifadhi wa bahari, Mratibu huyo alisema wanawake na vijana ndio nnguvu kazi kuu inayotumika katika uhifadhi wa bahari kwa upande wajamii.
Alisema katika kamati ya jamii kila moja ina wanawake na vijana, kwani wanawake wanaushawishi mkubwa katika jamii na vijana ndio nguvu kazi.
Hata hivyo alisema jumla ya kamati 35 za jamii, zimeanzishwa katika PECCA, huku kazi zake kubwa ni kuelimisha jamii namna bora ya kutumia bahari kwa vizazi vijavyo.
“Kama hatukuchukua hatua zinazostahiki rasilimali ya bahari, mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la watu, basi rasilimali hiyo inaweza kupotea, vijana wengi wanapomaliza skuli wanaelekea baharini na shuhuli za uvuvi zinaongezeka na bahari ikiwa ndio hiyohiyo.
Kwa upande wa mabadiliko ya Tabianchi, alisema hali ya sasa sio nzuri na sio mbaya sana, kwani katika uhifadhi wanakitu kimoja cha doria, kwani bado rasilimali nyengine zipo na hazijaharibiwa.
Alisema PECCA ilianzishwa kwa lengo la kuhifadhi rasilimali za bahari, ili ziwe endelevu kwa kizazi cha sasa na baadae, rasilimali hizo ni samaki, matumbawe, miti ya mikandaa na mwani.
MWISHO
Abdi Juma Suleiman