Monday, November 25

ZECO kuzalisha umeme wa nishati ya jua Zanzibar wa megawati 18

 

NA ABDI SULEIMAN.

SHIRIKA la Umeme Zanzibar (ZECO), limesema baada ya kumalizika kwa kazi ya uwekaji wa umeme wa jua katika kisiwa cha Njao na Kokota, sasa ni zamu ya mradi mkubwa wa umeme huo utakao zalisha megawati 18 Zanzibar.

mradi huo wa umeme wa jua wa kuzalisha megawati 18 unatarajiwa kukamilika 2025, utaweza kupunguza tatizo la upungufu na ukosefu wa umeme mara kwa mara.

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya shirika la Umeme zanzibar (ZECO) Azizi Said Alil, wakati alipokua akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya bodi hiyo, kutembelea miradi ya umeme wa jua kisiwa cha Kokota na njao.

Alisema miradi ya Visiwa ni uwekejazi mkubwa ambazo umefanywa na ZECO, kwani miradi hiyo kuona jinsi gani wanaweza kufikisha umeme huo kwenye maeneo ambayo umeme wa gridi hauwezi kufika.

Aidha alifahamisha kuwa mrida hiyo imegharimu fedha nyingi, dola laki nne za kimarekani zimetumika, huku akiwataka wananchi kuitumia fursa hiyo kwa kuunga umeme ndani ya nyumba zao.

“Tunapaswa kuishukuru serikali kwa kufanikisha juhudi mbali mbali, ZECO inawekeza nguvu kuhakikisha wananchi wote wananufaika na kupitia umeme wa jua,”alisema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa ZECO Zanzibar, Mshenga Haidar Mshenga, alisema umeme wa nishati ya jua hauna tafauti yoyote na umeme wa gridi, hivyo wananchi wasiogope kutumia na wanunue vifaa vyote vya umeme ni sawa tu.

Alisema umeme huo bado haujatumika kabisa, kwani haujafikia hata asilimia 3%, unatosheleza kuwekeza hata kama kuna wawekezaji wanaotaka kuekeza viwanda.

Akizungumzia mikakati ya shirika, alisema ni kuwaungia bure umeme wananchi wa visiwa hivyo, ili uweze kutumiaka na wananchi watalipia kidogo kidogo.

“Umeme mwingi unaozalishwa na matumizi bado ni madogo, ili mradi uweze kutikisika basi hata wananchi wote wakaungiwa huduma hiyo, itakua ni bado umebakia tukipata viwanda au wawekezaji tunaweza kufikia,”alisema.

Kwa upande wao wananchi wa visiwa hivyo wamishukuru serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuwakumbuka kwa kuwapatia huduma hiyo ya umeme ndani ya visiwa vyao.

Wamesema kuwepo kwa nishati hiyo itaweza kubadilisha maisha yao, kwani wananchi wa visiwa hivyo shuhuli zao kubwa ni uvuvi watautumia kwa kuhifadhi samaki wao na kuuza bei wanazotaka.

Tayari shirika hilo limeshafikisha huduma za umeme katika visiwa mbali mbali vidogo vidogo, Ikiswemo Kisiwa Panza, Makoongwe, Fundo, Uvinje, Kojani, Njao na kokota, ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo.

MWISHO