Thursday, November 14

TAMWA-ZNZ yatangaza awamu ya pili Tuzo za wanahabri Z’bar

 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Chama hicho wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja katika mkutano maalumu ulilenga kuzinduliwa kwa awamu ya pili ya tunzo za waandishi wa habari kuhusu wanawake na uongozi pamoja natakwimu.

Alisema pamoja na  jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na  Serikali  kuridhia mikataba ya kitaifa na kimataifa Pamoja na  malengo endelevu ya milenia na ASASI za kiraia zinazojihusisha na utetezi wa  haki za wanawake katika kuwajengea uwezo na kuwahamasisha kugombea nafasi mbalimbali.

Alisema bado takwimu  zinaonesha kuwa ipo namba ndogo  ya viongozi  wanawake katika ngazi mbali mbali ukilinganisha na wanaume katika nafasi za kiutawala  lakini Zaidi kwenye nafasi za kisiasa ambako bado kunaonekana mwanamke anakosa  fursa hasa katika nafasi za juu  zakushika uongozi katika miundo  ya vyama vya siasa vyenyewe  Pamoja na kuwa na  jumuiya za wanawake katika  vyama hivyo

Alieleza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha ni mawizi 6 tu wanamwake  kwenye idadi ya mawaziri 18 ambapo ni  sawa 33.3 % vile vile katika nafasi za ma naibu mawaziri ambapo   hadi sasa ni 1 kwenye idadi ya manaibu Waziri 7 ambapo ni sawa na    14.3 %, hali   hii pia inaonekana katika nafasi za makatibu  wakuu wakuu 5 tu kati 12 ambao  ni wanaume sawa na  29.4 % samba na wakuu wa mikoa  ni 1 tu ndio mwana mke kati ya 5 hali hii pia  imejitokeza pia katika ngazi za halmashauri na serikali za mitaa wawilaya  kwenye  viongozi wa shehia

Sambamba na hayo Mkurugenzi huyo alisema Chama cha waandishi wahabari waanawake Tanzania ofisi ya Zanzibar (TAMWA), ikishirikana na  Jumuiya wanasheria wanawake  (ZAFELA) na jumiya ya Utetezi wa jinsia na mazingira Pemba (PEGAO) kupitia  udhamini wa Ubalozi wa  Norwey nchini Tanzania inatekeleza mradi wa kuwainua  wanawake katika Uongozi (SWIL).

Aidha alisema kupitia   mradi huu wa kuwawezesha wanawake katika uongozi kwa  kiasi kikubwa  imeweza kulipa umakini wa karibu Zaidi , fursa uwezo, mapungufu juu ya jitihada kufikia kutambua usawa wa kijinsia  na uwewezashaji wa wanawake  hususan katika nafasi za uongozi .

Hata hivyo  kwa upande wa vyama vya siasa , baadhi ya vyama vimekuwa vikibana fursa kwa wanawake kuwapa nafasi za juu kuongoza kutokana na mifumo waliyonayo au kutokuwa na mikakati ya makusudi kwa kulizingatia suala la usawa wa jinsia katika nafasi za uongozi

Hivyo basi Pamoja na kuendesha shughuli mbalimbali   kupitia mradi huu TAMWA-ZNZ mwaka  2021  iliandaa mashindano ya uandishi mahiri  juu ya kuripoti  tawimu zinazohusiana na ushirikishwaji wa wanawake katika nafasi za uongozi   Zanzibar.

Lengo kuu La mashindano haya  ni kushajiisha  waandishi wa Habari kuandika Habari za umahiri ili kuhakikisha  tauluma ya umahiri Pamoja na mwamko katika fani ya Habari kwa kuzingatia  utambuzi wa vyombo vya Habari wenyewe juu ya dhamira ya TAMWA  katika kutetea haki za wanawake na Watoto  kwa kufanya  shughuli za kuengeza uwelewa  ikiwemo matumizi ya vyombo vya Habari kupitia  magazeti, televisheni, redio na mitandao ya kijamii.

Akifafanua Zaidi alisema katika zoezi hilo  lilifanikiwa  kuibua  na kuwapata washindi ambao ni waandishi  katika vyombo mbali mbali walioshinda  kutokana na kazi zao  zilizoshindanishwa  zilizozingatia matumizi sahihi ya takwimu, pamoja na vigezo vyengine vya habari za umahiri Zanzibar kupitia uanzishwaji wa tunzo ya uandishi wa habari ya “Sauti Yangu, Haki Yangu”  sambamba na kuwashajiisha wanahabari kuona umuhimu wa kuzingatia dhana hii katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku  ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wao  katika jamii na kuwafikia makundi yaliyo pembezoni  kuweza kupaza sauti zao kupitia vyombo vya Habari kwa  kuzingatia haki na usawa kijinsia.

Katika muendelezo wa shuguli za mradi  kwa mwaka huu   TAMWA ZANZIBAR imekusudia kuendesha  mashindano ya  Habari  zinazohusiana zinazohusiana na ushirikishwaji wa wanawake katika nafasi za uongozi   Zanzibar  na changamoto zinazokabili jamii katika kujenga jamii  ambayo inaheshimu  haki , heshima  katika usawa wa jinsia kwa kuzingatia makundi mengine yanayoishi na  mazingira magumu  na wanaotaka kusaidiwa kupaza sauti zao.

Katika mashindano  ya mwaka  2021 jumla ya   kazi 452  zilipokelewa, ambapo kazi 73 zilikuwa makala za magazeti, kazi 3 zilikuwa makala (documentaries) za televisheni, makala 116 zilikuwa za redio na makala 260  zilikuwa za mitandao ya kijamii kutoka vyombo mbali mbali  vya Unguja, na Pemba,  na kutolewa tuzo  kwa kila mshindi

Hata hivyo TAMWA Zanzibar  kwa kushirikiana na Jumuiya wanasheria wanawake  (ZAFELA) na jumiya ya Utetezi wa jinsia na mazingira Pemba (PEGAO) kupitia  udhamini wa Ubalozi wa  Norwey nchini Tanzania kupitia mradi wa SWIL inapenda kuwaalika na kuwataka ushiriki wao Waandishi wote kitaaluma na  wa kujitolea ambao huandikia magazeti  kutoka Unguja and Pemba  ambao Habari zao  wanachapisha  katika magazeti na Habari za kieletroniki kwa kuzisambaza  katika  maeneo mbali  mbali kwa kuwalenga   wahusika.

Vile vile TAMWA inawasisitiza  washiriki  wote walioshiriki katika shindano lilopita   ambao  alama zao hazikutosha kutumia fursa hii kuandika tena habari za umahiri zenye  dhumuni  linalohusiana  na  wanawake  na   uongozi kipindi cha mwaka  cha mashindano ya  2022 kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.

Akieleza kuhusu vigenzo vitakavyotumika katika kuhakiki kazi za waandishi na watayarishaji wa vipindi hadi kupata washindi, mbali ya kuzingatia vigezo vya kitaaluma na uandishi wa habari zenye umahiri, vigezo kadhaa kama vifutavyo,Ubora wa kazi  utakaowasilishwa  utaangaliwa uweledi, umahiri wa uandishi,Upekee wa mada ,Umuhimu wa kuzingatia uwiano wa usawa wa jinsia,vyanzo vingi vya habari vilivyojitawanya pamoja na ushirikishaji wa wananchi na  wadau(different sources)Ubunifu wa mada husika.

Mpangilio wa mada,Ufasaha na mtiririko wa lugha,Kuzingatia maadili ya uandishi wa habari,Uweledi wa matumizi ya takwimu,matokeo baada ya kutoka habari au kipindi hicho (impact) Kipindi cha Redio na Televisheni kisichozidi dakika 30 na kuzingatia ubora wa sauti na ubora wa picha.

Katika mashindano  ya mwaka  2021 jumla ya   Habari 452 zilikusanywa  kutoka vyombo mbali mbali  vya Unguja, na Pemba, Habari hizi ni kutoka magazeti ,radio,  televisheni  na mitandao ya kijamii  na kutolewa tuzo  kwa kila mshindi

Mradi wa kushajiisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia  ni mradi wa miaka minne (2020 – 2023), wenye lengo la kukuza ushiriki wa wanawake katika uongozi ambao unatekelezwa  na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) jumiya ya Utetezi wa jinsia na mazingira Pemba (PEGAO) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway chini Tanzania.