Thursday, November 14

WATAKIA kuepuka kujiingiza katika makundi hatarishi vijana

NA ABDI SULEIMAN.

WANANCHI wa shehia ya Wawi Wilaya ya Chake Chake, wametakiwa kufuatilia mienendo ya vijana wao, ili kuepuka kujiingiza katika tabia hatarishi ambazo zinaweza kuwapelekea kubaya.

Hayo yameelezwa na kaimu mratibu Tume ya Ukimwi Zanzibar Ofisi ya Pemba, Ali Mbarouk Omar katika mkutano wa uhamasishaji jamii juu ya masuala ya Tabia hatarishi, mkutano uliofanyika Wawi.

Alisema iwapo wazazi watakua makini na vijana wao, matukio maovu yanaweza kupungua na hata kujiingiza katika vikundi hivyo na kuepuka kuiga tabia hatarishi.

Aidha kaimu huyo aliwataka Vijana kujitahidi kuchunguza afya zao hospitali, kwa kuangalia maradhi mbali mbali ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana.

“Shehia hii imekua na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbali mbali, tabia zinabadilika sasa wazazi wakati wetu kuwa makini na vijana wetu ili wasiide tabia zilizokua sio nzuri,”alisema.

Alisema kua na maambukizi ya virusi vya ukimwi sio mwisho wa dunia wala sio kifo, kuna watu wanaishi na maambukizi miaka 25, lazima tuwe wajasiri wa kuchungua afya zetu mara kwa mara, pamoja na kutibu magonjwa ya kujamiana ukiyawacha utafanya hatari ya kuepelekea kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizunguzmia kuhusu watoto, alisema mtoto nzuri ni yule anaesoma tabia nzuri za wazazi wake, hivyo wazazi kuwa kiyoo kwa watoto wao, sambamba na kurudisha malezi ya pamoja katika shehia zao.

Kwa upande wake Ahmed Issa Mohamed, akizungumzia ugonjwa wa Kifua Kikuu, aliwataka wananchi kupima afya zao, kwani ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari na upo.

“Huu ni ugonjwa hatari sana nao, ugonjwa huu hautibiki kwa dawa za miti shamba bali dawa za hospitali ndio tiba pekee, hivyo ni vizuri kupima afya zenu,”alisema.

Naye msanii Abdalla Hamad (mzee mpemba),aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wa shehia, pale wanapowaona wageni wameingia katika shehia bila ya kibali cha sheha, pamoja na kutokua na maadili mauri kwa watoto wao.

Nao wananchi wa shehia ya Wawi Khamsi Juma Omar, aliwataka vijana kutambua thamani na utu wao katika jamii na taifa kwa ujumla, sambamba na kuacha kuiga mambo yasio kuwa na maana kwao.

Naye Nassor Said, aliwasihi wazazi kutokupatia furs asana watoto wao, badala yake kuwa makini nao ili kuwaepusha kuingia katika makundi hatarishi kwao.

MWISHO