Thursday, November 14

DC CHAKE CHAKE AZINDUA HUDUMA YA TELEZA KIDIJITALI

NA ABDI SULEIMAN

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, ameishukuru benk ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono juhudi mbali mbali za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ya kuwasaidia vijana wasio na ajira katika suala zima la kujiajiri wenyewe na kukuza kipato kwa walionacho.

Alisema ili kujikomboa katika uchumi na changamoto walizonazo vijana, kufungua akaunti katika benk ya NMB kwani wataweza kunufaika na huduma mbali mbali zinazotolewa na benk hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya aliyaeleza hayo wakati wa uzinduzi wa huduma ya TELEZA KIDIJITALI, kwa wananchi wa Wilaya ya Chake Chake na wafanyabiashara, halfa iliyofanyika katika soko la matunda Chake Chake, chini ya benk ya NMB Tawi la Pemba.

Alisema iwapo watafungua akaunti katika benk hiyo, wataweza kujikomboa kiuchumi katika ngazi ya mtu moja moja, shehia na familia.

“Sasa vijana tushindwe sisi wenyewe, njia tayari ya kutoka kimaisha ipo na wezetu NMB wameshatuletea, niwakati wa kuchangamkia fursa hii kwa haraka ili isije ikapotea,”alisema.

Aidha Mkuu huyo aliwataka vijana, wafanyabiashara na wananchi kuitumia fursa hiyo kwa kupata mikopo isiyonamasharti, ili tuweze kujikombo katika maisha yetu.

Alisema fursa hiyo ni adhimu sana hawapaswi kuiwacha na kuelekea kufeli, kwani NMB imekuja kuwatatulia matatizo yao, kwa lengo la kujenga kisiwa cha Pemba.

“Vijana wa Bodaboda, wavuvi, wakulima, wafanyabiashara hii ni fursa adhimu kwetu, tuitumie fursa hii kwa maslahi yetu na taifa ili tuachane na ukaaji wa vibarazani,”alisema.

Katibu Tawala Wilaya ya Chake Chake Suleiman Hamad Suleiman, alizitaka benk nyengine nazo kutoa fursa kwa vijana, ili waweze kungana na kauli ya Rais ya kuwapatia ajira laki 50000 wananchi.

“Fursa zinakuja na tunapaswa kuzichangamkia, vijana wengi wanahitaji kazi na kuwainua kiuchumi, vizuri tukazichangamkia wakati wenzetu nmb wamekuja kutuletea,”alisema,

Naye meneja wa biashara za NMB kanda ya Zanzibar Naima Said Shaame, aliwataka vijana kuzitumia fursa zinazoanzishwa na bank ya NMB, kwani uzinduzi wa TELEZA KIDIJITALI ni huduma maalumu zilizokuja karibu ya wananchi.

Alisema lengo la huduma hiyo ni kurahisisha maisha ya wananchi kwa ajili ya kupata huduma bora, huduma za haraka lakini huduma ukiwa na simu yako ya mkononi.

“Sote tunajuwa kauli ya Rais wetu wa Zanzibar ni kuifanya Zanzibar kuwa kidijitali, sisi kama bank tunamuunga mkono kwa kuleta huduma na lengo la Rais ikafikiwa”alisema.

Alifahamisha kuwa TELEZA KIDIJITALI inatoa huduma tatu, moja mshiko fasta uwe na akount ya NMB unaweza kukopa fedha ukiwa na simu yako ya mkononi kuanzia shilingi 1000 hadi laki 50000/=, bila ya kuwa na masharti yoyote.

Alisema huduma ya pili ni NMB Pesa wakala, ni wananchi wanaweza kuongeza bishara nyengine kwa kuwa na simu ya mkoni, simu hiyo itaweza kukusaidia kujiajiri mwenyewo.

Aidha huduma ya tatu ni lipa namba, baada ya kutembea na pesa mfukoni bali sasa fedha unalipia kuwa na simu na inawasaidia wafanya biashara kuongeza mzunguruko wake.

Kwa upande wake meneja wa NMB Tawi la Pemba Hamad Mussa Msafiri, aliwataka wananchi wa Wilaya ya Chake Chake kuitumia fursa ya TELEZA KIDIJITALI ili waweze kufikia malengo yao ya kibiashara na kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wao waendesha bodaboda Wilaya ya Chake Chake, wamesema huduma hiyo imewasaidia sana kwani vijana wataweza kupata bodaboda ambazo watazitumia kwa shuhuli zao za kujiajiri wenyewe.

Hata hivyo huduma hiyo itaweza kuwafikia wananchi wa Wilaya ya Mkoani, wete na Micheweni, itakumbukwa kuwa hivi karibuni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliizindua rasmi huduma hiyo mjini Unguja.