Friday, January 17

JET yawakutanisha wahariri tanzania kujadili masuala ya uhifadhi

       

NA ABDI SULEIMAN.

 

CHAMA cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET), kinatarajia kuwakutanisha wahariri wa Habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini, kwa lengo la kuwaongeza uwelewa juu ya masuala uhifadhi wa korido katika maeneo yanayounganisha wanyamapori, uhifadhi wa baharini na misitu, usafirishaji na ujangil, kukuza uhifadhi wa wanyamapori na utalii.

 

JET imesema kuwa jumala ya wahariri 25 kutoka vyombo mbali mbali vya habari, wataweza kubadilishana uzoefu ili kuweza kuzihakiki kwa uzuri habari zinazochapishwa na waandishi wao habari wanaoshiriki katika program za mafunzo kutoka JET.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa JET John Chikomo, alisema mkutano huo wa mashauriano na wahariri wa habari, utafanyika Bagamoyo-Millennium Sea Breeze Resorts Julai mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa Tuhifadhi Maliasili Tanzania unaofadhiliwa na USAID.

 

Aidha aliyataja malengo makuu ya mkutano huo ni pamoja na kuwa na ujuzi wa kutosha wa masuala ya uhifadhi wa korido katika maeneo yanayounganisha wanyamapori, uhifadhi wa baharini na misitu, usafirishaji na ujangil, kukuza uhifadhi wa wanyamapori na utalii.

 

Malengo mengine ni kuboresha ubora wa taarifa za vyombo vya habari kuhusu utunzaji wa korido/muunganisho wa wanyamapori na masuala mengine ya uhifadhi wa viumbe hai.

 

“Kupata ujuzi unaotaliwa kuwawezesha wahariri kusambaza kwa umma elimu waliopatiwa, ili makundi mbalimbali ya umma yaweze kuchukua hatua stahiki,”alisema.

 

Akizungumzia matarajio ya mkutano huo, Chikomo alisema waandishi wa habari wa Tanzania kupata uwezo na ujuzi wa masuala ya uhifadhi wa korido ili kuchunguza, kuripoti na kuchambua uhusiano wa wanyamapori.

 

Alisema vyombo vya habari vinatumia ujuzi uliopatikana wa uchunguzi na uchanganuzi ili kutoa mtiririko wa habari wa kuaminika wa mara kwa mara na wa uwazi kutoka kwa wananchi hadi watoa maamuzi na wadau wengine kuhusu utangazaji wa korido na unganisho wa wanyamapori na masuala ya uhifadhi wa  bayoanuai.

 

“Kumekua na mitandao inaundwa kuunganisha vikundi vya wahariri wa Tanzania katika ngazi ya wilaya na wenzao katika ngazi ya kitaifa, wanaoshughulikia masuala ya sekta ya wanyamapori nchini,”alisema.

 

Hata hivyo Mkurugenzi huyo, alifahamisha kuwa vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kutekeleza na kukuza maendeleo ya taifa kwa kuripoti habari zenye maslahi kwa umma na kuwawajibisha wale walio na mamlaka.

 

Chikomo alibainisha kuwa hilo ni Jukwaa la kwanza la wahariri kuhusu uhifadhi wa bayoanuai na taarifa za wanyamapori, litakaloendeshwa na JET likiwa na lengo la kuwapa waharirintaarifa yanayohitajika ili kushughulikia stori zinazowasilishwa na waandishi wao.

 

Mkutano huo utanatoa fursa kwa wahariri kurejea wajibu wao kuwaunda waandishi wa habari kuwa vazi ambalo kazi yake italeta mabadiliko katika jamii kupitia matumizi ya busara ya mapato ya utalii.

 

 

MWISHO