Thursday, January 16

VIDEO: Akinamama wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi wameshauriwa kujiunga na huduma za uzazi wa mpango 

 

Na Raya Ahmada.

Akinamama wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi wameshauriwa kujiunga na huduma za uzazi wa mpango ili kuepuka kuzaa papo kwa papo ambayo inaweza kupunguza kwa kinga mwilini ambayo inahatarisha kupata magonjwa nyemelezi na hata kumuambukiza mtoto.

 

 

 

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mratibu wa Tume ya UKIMWI ofisi ya Pemba Ali Mbarouk Omar wakati akizungumza na ZBC ofisini kwake Chake chake.

 

Amesema akinamama wanapoingia katika huduma hiyo wanapewa ushauri wa kuzaa watoto wanaopishana ili kujipunguzia mzigo wa kupoteza nguvu kwa kujifungua mara kwa mara.

 

Kwa upande wake Msimamizi wa vituo vya klini za huduma na tiba kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi kanda ya Pemba dk. Rahila Salum Omar amesema mama hao kupumzika kwa miaka miwili au zaidi itarudisha hali za afya zao sambamba na kuwatunza watoto wao.

 

Nae Maryam Said Abdalla ambae anaishi na virusi vya ukimwi amesema huduma hiyo ni muhimu kwao kwani kinga zao zinaposhuka hata fuko la uzazi linaweza kupata maambukizi.

 

ANGALIA VIDEO HII KWA KUBOFYA HAPO CHINI