Thursday, January 16

HABARI PICHA: KAMISAA wa Sensa ya watu na Makaazi Zanzibar Akutana na waandishi wa habari Pemba.

KAMISAA wa Sensa ya watu na Makaazi Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza, akifungua mafuzo ya siku moja kwa waandishi wa habari Pemba, juu ya uhamasishaji wa sense ya watu na Makaazi mwaka 2022, mkutano uliofanyika mjini Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
AFISA Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau, akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa sense ya watu na makaazi kwa waandishi wa habari Pemba, mkutano uliofanyika mjini Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
BAADHI ya waandishi wa habari kutoka Vyombo mbali mbali vya habari Pemba, wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo ya uhamasishaji wa Sensa ya watu na Makaazi kwa waandishi wa habari, mkutano uliofanyika Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
MTAKUWIMU kutoka Ofisi ya Mtakuwimu Mkuu wa Serikali Said Mohamed Saidi, akiwasilisha mada katika mkutano wa waandishi wa habari, juu ya uhamasishaji wa sense ya watu na makaazi mkutano uliofanyika mjini Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)