Thursday, January 16

Mafanikio utekelezaji mradi wa SWIL Z’bar yaanza kuonekana

Afisa Ufuatiaji na Tathmini kutoka TAMWA-ZNZ Mohamed Khatib akifafanua jambo katika mkutano uliowashirikisha wahamishaji jamii mbali mbali kutoka Unguja na Pemba.
Mhamasishaji jamii kutoka Pemba Ali Abdalla Juma akitoa ushuhuda kama sehemu waliokua wakikutana nayo katika uhamaishaji jamii.
Fransisca Camilius kutoka Magharib A Uunguja akiwasilishaji ripoti ya miezi sita ya utekelezaji mradi huo.
Mhamasishaji jamii kutoka mjini Imran Mohamed akiwasilishaji ripoti ya utekeleza mradi huo wakati wa uhamaishaji kwa miezi sita.
Miongoni mwa wahamasishaji jamii kutoka Unguja na Pemba wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa ripoti za utekelezaji kwa miezi sita.

NA MWANDISHI WETU.

Uwepo wa utekelezaji Mradi wa uhamasishaji Wanawake katika uongozi (SWIL) unatajwa kuwa mwarubaini unaochechea uwajibikaji kwa viongozi katika kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

Wakiwasisilisha ripoti ya miezi sita kutoka  mwezi Januari hadi Juni mwaka huu wahamaisishaji jamii (CBs) wamesema wakati wanaanza kazi ya uhamasishaji huo walikuta changamoto nyingi zinazowakabili wananchi huku na baadhi wakishindwa kupaza sauti zao na kutojua nini la kufanya.

Mkutano huo wa uwasilishwaji wa taarifa za utendaji kazi umefanyika katika Ukumbi wa skuli ya Jangombe na kuhudhuriwa na wahamasishaji hao kutoka Unguja na baadhi kutokea Pemba.

Mmoja miongoni mwa washiriki hao kutoka Wilaya Mjini Unguja Imran Mohamed alisema walipokwenda Shehia ya Mlandege wananchi walilalamika sana kuhusu ukosefu wa huduma ya maji safi na salama na kupitia taarifa hizo walifanikiwa  kutengeneza ushawishi mkubwa hatimae changamoto hio imetatuliwa na Mbunge wa jimbo la mji Mkongwe Mohamed Suleiman baada ya kuwekwa kikao maalumu cha pamoja na wananchi wa shehia hiyo.

Alisema hapo awali kwa muda mrefu wananchi wa eneo hilo walikua wakikosa huduma hio na kupitia wao (CBs) wamekua sababu ya kumfanya Mbunge wa jimbo hilo kutoa vifaa mbali mbali ambavyo vimesaidia kutatua changamoto hiyo.

Sambamba na hayo aliongezea katika miezi hiyo sita pia  wameweza kuwajengea uwezo wanawake wengi kusimama na kupaza sauti kueleza hisia zao, utaratibu ambao hawakuwahi kuwa nao kwenye maisha yao yote hapo awali.

Alisema anaamini kupitia mradi huo  uwajibikaji mkubwa utaongezeka na kukuza maendeleo kuanzia ngazi ya shehia na hadi Taifa sambamba na ushiriki wa wananwake  wengi zaidi katika kugombea nafasi za uongozi.

Mhamaishaji mwengine Moza Rashid alisema katika maeneo mengine wananchi bado hawana vitambulisho vya mzanzibari mkaazi huku wakidai uwepo wa changamoto ambazo zinawakwamisha kupata  vitambulisho hivyo.

Alitolea mfano shehia ya kikwajuni mjini Unguja katika mikutano yao waligundua watu 34 walibaini hawana vitambulisho vya mzanzibar  na kueleza changamoto tofauti wanapofuatilia vitambulisho hivyo.

Akifafanua zaidi alisema kupitia mradi huo waliweza kuwasaidia wananchi hao 34 na kati yao hadi sasa zaidi watu 10 tayari wameshapata vitambulisho hivyo kwa hatua ya awali huku wengine wakiendelea na mchakato na anaamini katika siku za hivi karibuni na waliobaki pia watapatiwa vitambulisho hivyo.

Nae Fransisca Camilius kutoka Magharib A Uunguja alisema katika Shehia ya Bumbwisudi Jimbo la Mfenesini wananchi walijengewa uwezo na hatimae kupaza sauti zao kueleza changamoto ya Mbunge wa jimbo hilo kutoonekana kabisa katika shehia hiyo.

‘’Sisi kama CBs tulifanya mawasiliano na Mbunge husika ambae ni Zubeida Khamis Shaibu  alikiri changamoto hio na muda mfupi alianza kuifanya kazi na mpaka kutoa ahadi ya kujenga ofisi ya Mbunge katika shehia hiyo’’alisema.

Mradi wa uhamaishaji wanawake kushiriki katika nafasi za uo ngozi (SWIL) Zanzibar unatekelezwa na TAMWA-ZNZ,ZAFELA pamoja na PEGAO kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.