NA ABDI SULEIMAN.
KAMISHNA wa Sensa ya watu na Makaazi Tanzania Upande wa Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza, amesema Sensa ya mwaka 2022 haina ubagauzi na wamejipanga kuwahesabu wananchi wote yakiwemo makundi maalumu.
Alisema zoezi hilo limepangwa kuwahesabu wananchi wote hadi wageni waliolala ndani ya nchi, ikiwemo watu wenye ulemavu ili viongozi kuweza kuifikisha taarifa kwa wengine.
Kamishna huyo aliyo aliyaeleza huko ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake, wakati alipokua akifunguza mafunzo ya uhamasishaji wa sense ya watu na makaazi kwa watu wa makundi maalumu wakiwemo wenye umelavu.
Alisema dhumuni la serikali ni kuhesabu watu wote hakuna mtu atakaebakishwa, mkazo umewekwa kwa watu wenye mahitaji maalumu hasa walemavu, hivyo viongozi wa taasisi hizo wanapaswa kushirikiana na serikali katika hilo.
“Hakuna mtu asienahaki ya kuhesabiwa asifichwe mtu, viongozi kushirikiana na serikali, imepanga mipango maalumu kwa watu wenye mahitaji maalumu,”alisema.
Alifahamisha kuwa niwajibu kwa viongozi wote kushirikiana na serikali, katika kuelimishana ili kuona wananchi wote wanahesabiwa, na serikali iweze kutoa huduma kulingana na idadi ya watu.
Aliwataka viongozi kuzungumza na watu wao ili zoezi hilo liweze kutimia na kuhesabiwa, kwani suala la sensa linamuhusu kila mtu kuhakikisha kwamba anafanikisha suala hilo.
Hata hivyo alisema sense ya 2022 ni sense ya sita (6) kufanyika tokea kupatikane uhuru, Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni sensa maalumu ipo katika kiwango cha maendeleo ya hatua ya katitaki kiuchumi.
“Sense ni jambo muhimu sana kwa kila nchi, nchi zoete duaniani zinafanya sensa kwa kipindi walichojiwekea wenyewe, Zanzibar inafanya kila baada ya miaka 10, nchi nyengine zinafanya kila miaka mitano inategemea na uwezo,”alisema.
Aliongeza kuwa taarifa za sense hutumika kwa ajili ya kupanga maendeleo ya nchi, kupanga miradi ya maendeleo kama vile elimu, barabara, maji, umeme na kufanya maamuzi na kupima utekeleza wa mambo mbali mbali,
Alisema Serikali nayo inapanga matumizi yake na bajeti yake katika ngazi ya shehia, jimbo, wilaya , mkoa na taifa na inagawa rasilimali zake.
Mkurugenzi wa baraza la taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar Ussi Khamis, alisema jukumu la baraza ni kuratibu masuala yote ya watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanashiriki mkikamilifu katika suala zima la sense.
Alisema zoezo la sensa ni la kitaifa wajibu kila mmoja kuhesabiwa ili serikali iweze kujuwa takwimu za watu wake katika kupanga miradi ya maendeleo.
Aidha alisema watu wenye ulemavu wanawajibu wakuhesabiwa, hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanawatoa watoto wenye ulemavu ili kuhesabiwa na sio kuwaficha majumbani.
Kwa upande wake Mudathir Shaib Khamis, aliipongeza Serikali ya SMT na SMZ, kwa kuwajali watu wenye ulemavu na kuona wanaumuhimu wa kuhesabiwa.
Naye Mohamed Toli, aliwataka watu wenye ulemavu kuhakikisha wanakua mstari wambele kuhesabiwa siku hiyo, sambamba na kutokuwaficha watoto hao.
MWISHO