RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:Samia Suluhu Hassan, amewasili Kisiwani Pemba akitokea kisiwani Unguja kwa ziara ya siku mbili kisiwani humo.
Rais Samia aliwasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Air port na kupokealewa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi mbali mbali wa Vyama vya siasa, wabunge, wawakilishi, wananchi.
Mara baada yakuwasili kisiwani hapo aliweza kupata burudani mbali mbali kutoka kikundi cha sanaa Mkota ngoma ya Mkoani, Kiumbizi Pujini na Brasbend ya Vijana Pemba.
Kwamujibu wa raiba yake iliyotolewa kwa ajili ya Ziara hiyo, Rais Samia ataswali swala ya Ijumaa katika mskiti wa Masjid Taqwa Gombani Wilaya ya Chake Chake.
Aidha Rais Samia Julai 16 atakuwa na mazungumzo na wazee wa vyama vya siasa na viongozi wa dinia Kisiwani Pemba, kikao kitakachofanyika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma alisema ujio wa Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa ni kuonyesha ushupavu wa siasa, kwani ndio Rais wa Wawatanzania Wote.
Alisema kujakwe ni kuashiria maendeleo mazuri na makubwa yaliyofikiwa katika kisiwa cha Pemba katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya Nane ya Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
“Sisi chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba, tumefarajika sana na ujuo wake na kumuomba kutokuchoka kuwatembelea wananchi wa kisiwa hichi,”alisema.
Naye Juma Omar mkaazi wa Mkoani, alisema hii ni mara ya kwanza katika miaka hii ya 2000 kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulala ndani ya kisiwa cha Pemba, yote ni kuashiria kuwa kisiwa cha Pemba kimo salama.
Alisema Kisiwa cha Pemba sasa kip[o katika hali nzuri ya utulivu na amani, hivyo kulala kwake kutaweza kuwaminisha viongozi wengine wa Tanzania kwamba Pemba ni sehemu sahihi nazuri kwa kupumzikia kama ilivyo Unguja.
Hata hivyo aliwataka wananchi wenzake na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa kuendelea kumuunga Mkono Rais Samia katika mikakati yake ya kuinua visiwa vya unguja na Pemba kiuchumi.
MWISHO