Thursday, January 16

UWANJA wa Michezo Gombani kufanyiwa matengenezo makubwa kugharimu Bilioni 2.8

AFISA Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau, akizungumza katika mkutano wamakabidhiano ya matangenezo ya Uwanja wa Michezo Gombani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja huo Chake Chake.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN,PEMBA)
MKANDARASI wa Ujenzi kutoka Kampuni ya OSAJU CO.LTD Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ussi Salum Pondeza, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa matengenezo ya uwanja wa Michezo Gombani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja huo Chake Chake.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN,PEMBA)
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Khamis Abdalla Said, akizungumza katika mkutano wa makabidhiano ya Uwanja wa Michezo Gombani na mkandarasi wa matengenezo ya uwanja huo, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja huo Chake Chake.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN,PEMBA)
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Khamis Abdalla Said (kushoto), akimkabidhi vielelezo vya matengenezo ya uwanja wa michezo Gombani mkandarasi kutoka Kampuni ya OSAJU.CO.LTD mkurugenzi wa kampuni hiyo Ussi Salum Pondeza, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja huo Chake Chake.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN,PEMBA)

NA ABDI SULEIMAN

WIZARA ya habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar imeukabidhi uwanja wa Michezo Gombani, kwa mkandarasi wa Ujenzi kutoka Kampuni ya OSAJU CO.LTD, kwa ajili ya kuufanyia matengenezo makubwa uwanja huo.

Uwanja huo wa gombani ambao unatarajiwa kufanyia marekebisho makubwa hivi sasa, katika ameneo mbali mbali ikiwemo kuwekwa tatani, nyasi bandia sehemu ya kuchezea, taa, ubao wa matangazo uwanjani hapo, vyumba vya wachezaji, kupakwa rangi upya, maboresho ya ukumbi wamikutano na kuongezwa ukubwa wa paa.

Makabidhiano hayo ya ujenzi huo umefanyika katika ukumbi wa uwanja wa michezo Gombani, nakuhudhuriwa na watendaji kutoka vitengo mbali mbali vya wizara ya habari Pemba.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Khamis Abdalla Said, alisema uwanja wa Gombani ulijengwa na wakorea ni miaka 30 sasa imepita na haukuwahi kufanyiwa matengenezo makubwa.

“Sisi Serikali tumeona ipo haja ya kufanyiwa matengenezo makubwa, ili kukudhi mahitaji ya sasa na baadae, pamoja na ilani ya CCM, tunahitaji kuwa na viwanja vya viwango vya kimataifa, ili uweze kutumika kwa mashindano ya kimataifa,”alisema.

Alifahamisha kuwa Serikali imefanya maamuzi makubwa kwa lengo la kuendeleza michezo Ungja na Pemba, matarajio ya serikali ni makubwa ni kufanywa kazi kwa ubora na makubaliano ya mikataba, hivyo mkandarasi anapaswa kujitahidi kwa kile walichokubaliana.

Hata hivyo alimtaka mkandarasi huyo, kufanya kazi kwa muda unaotakiwa, Rais anasisitiza wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati na ubora.

Naye Mkandarasi wa ujenzi huo kutoka kampuni ya Ujenzi ya OSAJU CO LTD, mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ussi Salum Pondeza, alisema wapo tayari kuifanya hiyo kazi kwa viwanga ambavyo wamekubaliana.

“Tumekuja hapa kukabidhiana baada ya kusaini mikataba na kuoneshana maeneo ambayo yote yamondani ya mkataba, na kujua kile ambacho tunakifanyia kazi,”alisema.

Alisema ushirikiano ndio muhimu sana katika kazi zao, wala hawatokuwa na uchoyo katika kazi hizo, wanatarajia kuifanya hiyo kazi kwa muda waliokabidhiana.

Aidha alisema kuna baazi ya vitu lazima wasghirikiane na Mshauri mwelekezi, kabla ya ujenzi haujaanza ili kuona uwanja huo unakuwa bora kama ilivyo viwanja vyengine.

Kwa Upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau, alimtaka mkandarasi huyo kutoa mashirikiano ya dhati na ofisi yake, ili kurahisisha hilo jambo ili liende kulingana na malengo yaliokusudiwa.

Alisema kuna baadhi ya wakandarasi wanapewa kazi Pemba, baade wanafanya maongezi na viongozi waliopo unguja wakati wasaidizi wao wapo pemba, jambo linaloleta sitofahamu baina ya taasisi na mkandarasi.

Hata hivyo alisema uwanja huo unatarajiwa kutumika kwa ajili ya siku ya mazoezi Januari Mosi 2033, hivyo kuhakikisha unakamilika kabla ya tarehe hiyo.

Naye mshauri Mwelekezi kutoka Azam fc injinia Victor Ndozero, alisema kukamilika kwa uwanja huo utaweza kutuwavutia hata FIFA na kuutumia kwa mashindano yao, kutokana na ukubwa wake na ubora utakaokuwa nao.

Jumla ya shilingi Bilioni 2.8 zinatarajiwa kutumiwa katika matengenezo ya uwanja wa Michezo Gombani, fedha kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

MWISHO

Abdi Juma Suleiman

Journalist/Photographer

Zanzibarleo newspaper
Chake Chake -Pemba
+255774565947 or +255718968355
+255622161506