Thursday, January 16

SAKHO AWASHUKURU WATANZANIA, MASHABIKI WA SIMBA AKABIDHIWA TUZO NA OKOCHA

HATIMAYE mchezaji wa timu ya Simba na raia wa Senegal, Staa Pape Sakho bao lake alilofunga mbele ya ASEC Mimosas, limeweza kuwa bao bora la CAF.

Hatua hiyo imekuja baada ya mchujo mkali kwa kupitia kura na Julai 21 aliweza kutangazwa mshindi kwa kuwashinda washindani wake ambao aliingia nao tatu bora.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo nchini Morocco ambapo aliweza pia kukutana na staa Sadio Mane raia Pape alishukuru kwa kusema “Asanteni Watanzania, asanteni mashabiki wa Simba, asanteni wachezaji wote, nimefurahi sana.”

Sakho baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Bao Bora la CAF alikabidhiwa tuzo hiyo nchini Morocco na Legend wa mpira barani Afrika Jay Jay Okocha

Ikumbukwe kwamba bao hilo alipachika kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Uwanja wa Mkapa mbele ya ASEC Mimosas na Simba ilishinda mabao 3-1.

Ni Zouhair El-Moutaraji  alifunga kwenye mchezo wa Wydad vs Al Ahly na Gabadinho Mhango mchezo wa Malawi vs Morocco hawa walikuwa ni washindani wake.

Katika sherehe za utoaji wa Tuzo hizo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) usiku wa Alhamisi mjini Rabat nchini Morocco, Sakho ameshinda dhidi ya Gabadinho Mhango wa Malawi na Orlando Pirates na Zouhair El Moutaraji wa Morocco na Wydad Athletic alioingia nao Fainali.

Sakho alifunga bao hilo dakika ya 12 tu akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe katika ushindi wa 3-1 dhidi ASEC Mimosas  ya Februari 13, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao mengine ya Simba siku hiyo yalifungwa na Kapombe dakika ya 79 na winga Mmalawi, Peter Banda dakika ya 81 akimalizia pasi ya Nahodha, John Bocco, wkaati bao pekee la ASEC lilifungwa na Stephane Aziz Ki 60 dakika ya 60.Senegal & Simba)
Washindi wengine wa tuzo za CAF mwaka huu ni nyota wa Senegal aliyejiunga na Bayern Munich akitokea Liverpool, Sadio Mane ambaye amebeba tena Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mbele ya mwananchi mwenzake, kipa Edouard Mendy wa Chelsea na Mohamed Salah wa Misri na Liverpool.

Ulikuwa usiku mzuri, baada ya Wasenegal wengine kubeba tuzo, Aliou Cisse akichukuwa ya Kocha Bora wa Mwaka na Pape Matar Sarr wa Tottenham Hotspur akiondoka na ya Mwanasoka Bora Chipukizi.
Asisat Oshoala wa Nigeria ameshinda kwa mara ya tano ya rekodi Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike, huku Senegal ikishinda tuzo ya timu Bora ya Taifa na Wydad Athletic ikibeba Tuzo ya Klabu Bora ya Wanaume na Mamelodi Sundowns Klabu Bora ya Wanawake.

WASHINDI WOTE TUZO ZA CAF

BAO BORA LA MWAKA

Pape Ousmane Sakho (Senegal & Simba)

MWANASOKA BORA WA MWAKA WA KIUME

Sadio Mane (Senegal and Bayern Munich)

MWANASOKA BORA WA KIKE

Asisat Oshoala (Nigeria and FC Barcelona)

MCHEZAJI BORA WA KIKE WA KLABU

Evelyn Badu (Ghana & Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)

MCHEZAJI BORA WA KIUME WA KLABU

Mohamed El Shenawy (Egypt & Al Ahly)

MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIKE

Evelyn Badu (Ghana & Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)

MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIUME

Pape Matar Sarr (Senegal and Tottenham Hotspur)

KOCHA BORA WA MWAKA MWANAMKE

Desiree Ellis (Afrika Kusini)

KOCHA BORA WA MWAKA MWANAUME

Aliou Cisse (Senegal)

KLABU BORA YA MWAKA YA WANAWAKE

Mamelodi Sundowns (South Africa)

KLABU BORA YA MWAKA YA WANAUME

Wydad Athletic Club (Morocco)

TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME

Senegal

TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME

Itapatikana baada ya Fainali ya Afrika za Wanawake zinazoendelea Morocco