Thursday, January 16

KUKHAWA yahimiza njia mbadala utatuzi migogoro

NA ABDI SULEIMAN.

JUMUIYA ya kupunguza Umaskini na kuboresha hali za wananchi Pemba(KUKHAWA), imesema wananchi wanapaswa kutumia mbinu mbadala za kusuluhisha migogoro inapotokea katika jamii na sio kukimbilia posli, jambo mbalo linaweza kupeleka uvunjifu wa amani.

Aidha alifahamisha kwamba migogoro inapotokea katika jamii jambo la busara ni kusuluhishana wenyewe kwa wenye, kwa kutumia viongozi wa shehi ili pande zote kupata haki zao, kwani wanapokwenda kwenye vyombo vya sheria amani inaweza kuvunjika.

“Wakienda Polisi basi mmoja wao lazima atakosa haki yake yote, au atapata pungufu mwisho wasiku uhasama ndipo unapoanzia, sio busara kukimbilia huko,”Kukhama imesema.

Akizungumza wakati waufunguzi wa mkutano wa utatuzi wa Migogoro inapelekea uvunjifu wa amani, mjini Chake Chake mratibu wa Mradi huko Zulekha Maulid Kheir, alisema wakati umefika kwa wanajamii kutumia njia hizo kabla ya kukimbilia polisi.

“Unajua kuna watu bado hawajarithishana ikifika kipindi cha karafuu wanakamatiana mapanga, wapo watu wanaharibiana vipando migomba, mikarafuu au miti mengine, matukio hayo yanapaelekea uvunjifu wa amani,”alisema.

Alisema zipo njia nyingi hutumika katika kusuluhisha hiyo migogoro, migogoro inayotokana na masuala ya ardhi hasa kipindi cha msimu wa karafuu, hali iliyopelekea kuziingiza shehia tanao nazo ni chonga, shungi, kilindi,Mgelema na Matale.

Aidha alisema migogoro inapotokea na watu kupelekeana polisi,  amani inakua haipo na amani inapotea, hali iliyopelekea kuwashirikisha masheha na wajumbe wa kamati zao katika mafunzo hayo.

Akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro mwanasheria wa kujitegemea Halfani Amour Mohamed, alisema suala la migogoro ilikuwepo tokea krane na karne zilizopita na ikisababishwa na kilimo, ufugaji na mambo mengine.

Alisema migogoro inayotokea hivi sasa inasababishwa na udhalilishaji, siasa, kiuchumi na ardhi, huku ardhi ikiwa ni sababu kubwa katika migogoro hiyo katika jamii kutokea na kupelekea uvunjifu wa amani.

“Tunapaswa kutumia njia mbadala katika kutatua migogori na sio kwenda polisi, vikao kwa sheha na kamati zake hapo haki itapatikana na hukatapeleka uvunifu wa amani,”alisema.

Akichangia katika mkutano huo, Maulidi Kheir Zubeir alisema migogoro inapotokea na busara isipotumika baadhi ya wananchi hukosa haki stahiki baada ya kwenda kwenye vyombo vya sheria.

Aidha alisema imefika wakati kwa wadau washeria kupita katika shehia mbali mbali na kutoa elimu kwa wananchi juu ya mbinu mbadala za kutatua migogo inapotokea katika jamii.

MWISHO