Wednesday, January 15

HATIMAE SIMBA WAZINDUA JEZI ZAO LEO

LEO Agosti 7,2022 washindi wa pili ndani ya Ligi Kuu Bara,Simba wamezindua uzi wao mpya ambao utatumika kwa msimu wa 2022/23.

Ni Sinza,madukani ilipo ofisi ya mdhamini wa Simba, Fred Vunjabei uzinduzi huo umeweza kufanyika.

Pia VunjaBei ametambulisha logo (chapa) mpya itakayotumika kutambulisha mavazi ambayo atakuwa anayazalisha kuanzia sasa, na kwa mara ya kwanza logo hiyo mpya ya VunjaBei Sports imeanza kuonekana kwenye uzi mpya wa Simba.

Kesho Agosti 8.2022 ni kilele cha Wiki ya Simba ambapo tamasha lao la Simba Day linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa.

Katika tamasha hilo Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya St George ambao tayari imeshawasili Tanzania.

Uzi mweupe wakiwa ugenini na ule wa rangi nyekundu wakiwa nyumbani.