Monday, September 16

KAMATI yaishauri Wizara kufuatilia bidhaa za wajasiriamali

BAADHI ya watendaji kutoka Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Taarifa ya utekelezaji wa bajeti kuhusiana na vikundi vilivyowezeshwa na wizara hiyo kipindi robo ya nne kuanzia April hadi Juni 2022, kwa wajumbe wa kamati ya Ustawi wa Jamii ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, hafla iliyofanyika Gombani Chake Chake Pemba
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, akisoma taarifa ya utekelezaji wa bajeti kuhusiana na vikundi vilivyowezeshwa na wizara hiyo kipindi robo ya nne kuanzia April hadi Juni 2022, kwa wajumbe wa kamati ya Ustawi wa Jamii ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, hafla iliyofanyika Gombani Chake Chake Pemba
AFISA Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau, akichangia jambo mara baada ya kuwasilishwa kwa taaira ya bajeti kuhusiana na vikundi vilivyowezeshwa na wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba, kipindi cha robo ya nne kuanzia April hadi Juni 2022, kwa wajumbe wa kamati hiyo, hafla iliyofanyika Gombani Chake Chake Pemba

 

NA ABDI SULEIMAN.

KAMATI ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, imeitaka Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba, kufuwafuatilia wajasiriamali wa bidhaa za mkono, ili kuwasaidia katika suala zima la umaliziaji wa bidha hizo kuhakikisha zinakua na ubora wa hali ya juu kabla ya kuziingiza sokoni.

Wajumbe wa kamati hiyo wamesema wajasiriamali wa bidhaa hizo Unguja na Pemba, wamakwama katika sehemu ya umaliziaji (finishing) wa bidhaa zao, katika kuwavutia wateja licha ya kua bidhaa hiyo ni bora na nzuri.

Wakizungumza mara baada ya kupokea ripoti ya Robo ya nne ya kuanzia April hadi Juni 2022, kwa wajumbe wa kamati ya Ustawi wa Jamii ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, hafla iliyofanyika Gombani Mjini Chake Chake.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mwantatu Mbarak Khamis, alisema vijana wamekua wakijitahidi katika utengeneza bidhaa mbali mbali lakini zinakosa kuwa na tija kutokana na kukosa ubora katika hatua za umaliziaji.

“Bidhaa zao ni nzuri unakuta mkoba mzuri lakini umaliziaji wake katika suala la upakaji wa rangi, hapo ndipo kikwazo kikubwa sana kwao, Wizara lazima kuingia kati suala hili ikizingatia kazi kubwa wanayoifanya lazima hapa tuwafikirie,”alisema.

Kwa upande mwengine, alisema vijana wanapaswa kuelimishwa juu ya kubuni miradi yenye tija kwao, inayoendana na maeneo yao husika pamoja na kuondosha changamoti za masoko, kwani wanapaswa kufikiria masoko ili wakivuna isiwe tabu kwao.

“Serikali kazi yake ni kuwasaidia wajasiriamlia na sio kuwatafutia masoko ya kuuza bidhaa zao, lazima wakubalia kuiondosha changamoto hiyo,”alisema.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mohamed Ahmada Salim, aliishauri Wizara ya habari kuwafauatilia kwa wanaotoa mikopo kuhakikisha wanawapatia kwa asilimia 1100 na sio kuwapatia asilimia 50 jambo ambalo halitishelezi kwao.

Hata hivyo aliitaka Idara ya Maendeleo ya Vijana kufuatilia kufuatilia CRDB kwa lengo la kujiridhisha juu ya taratibu za utoaji wa mikopo kwa kuwapatia wananchi kima kidogo kulingana na wanavyoomba.

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo Abdalla Abas Wadi, alisema Wizara inapaswa kufanya maboresho zaidi katika kusala la kuwapatia mikopo, pamoja na kuwafahamisha juu ya taratibu za urudishaji mikopo hiyo.

Hata hivyo kamati imeishauri wanapatiwa mikopo kupatiwa taaluma zaidi, ili mikopo waweze kutumiwa na kutumika iapasavyo na waweze kuirudisha kwa wakati.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, alisema wizara imekua mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana na kuona wanafikia malengo yao.

Alisema vijana wameamua kujiunga katika vikundi mbali mbali, kupitia fedha za COVID 19 vijana wengi wameshajihishika kuomba mikopo kwa wingi kupitia benk ya CRDB.

Naye Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Zanzibar Shaib Ibrahim Mohamed na katibu Mtendaji wa baraza la Vijana Zanzibar Salum Issa Ameir, wamesema bank ya CRDB imekua na changamoto katika utoaji wa mikopo kwa wajasriamali kwani wanashindwa kuwapatia mikopo kwa asilimia 100/% baadae huwapatia asilimia 50%.

Kwa upande wao viongozi wa vikundi vya Vijana Pemba, wameiyomba serikali kuingia kati utolewaji wa mikopo na CRDB kwani imekua na usumbufu mkubw akwa wajasiriamali.

Wamesema inawafika wakati wanaona bora kurudisha fedha wanazopatiwa, huku baadhi yao wakihiyari wasikope kwa kuepuka usumbufu wanaoupata sasa.

MWISHO