NA ABDI SULEIMAN
MKUU wa Wlaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, amesema Vijana wa bodaboda na wanamichezo Kisiwnai Pemba, wanapaswa kujikinga na kujilinda dhidi ya maambukizi virusi vya Ukimwi yasiendelee kutokea.
Alisema vijana hao shuhuli zao wanazozifanya ni ngumu na wanakutana na mambo mengi, kwani inafika wakati hukubali kulipwa fidia na abiria wao wanaowapakia bila kujali afya zao.
Mkuu huyo aliyaeleza hayo alipokua akizungumza na vijana wa bodaboda na wanamichezo, katika bonanza la uhamasishaji na upimaji wa VVU kwa vijana na kufanyika katika viwanja vya Gombani.
Aidha aliwataka vijana kuendelea kuchukua tahadhari, ili kuepuka maambukizo mapya ya ukimwi, ili waweze kujenga uwelewa kwao na kuwa wazalishaji wazuri na wanaoweza kufanya kazi vizuri.
Akizungumzia lengo la bonanza hilo, alisema ni mpango wa kuwaweka vijana katika kampeni ya kijana kataa ukimwi, pamoja na kuwahamasisha vijana kupakia abiria salama na kuchukua tahadhari ya kujikinga na Ukimwi.
“Ukimwi bado upo na utaendelea kuwepo, vijana na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari, mara nyingi ukimwi unazungumzwa kwa kutimia alama ya asilimia na watu wanashindwa kutafautisha, bora kutumia nambari moja kwa moja na watu watajua nini madhara yake,”alifahamisha.
Hata hivyo alisema Takwimu zinaonyesha makundi ya watu na baadhi ya maeneo mahususi yameripotiwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizo ya virusi vya ukimwi, kutoka na masuala mazima ya kujamiana.
Kwa upande wake Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza Pemba Ahmed Aboubakar, alisema vijana wa bodaboda wanapaswa kujisaidia na kusaidia ili kuepuka maambukizi mapya ya VVU nchini.
“Wapo baadhi ya abiri wanaopakiwa wanakua hawana fedha, baada ya kufikisha maeneo yao vijana wa bodaboda hujilipa jambo ambalo hinalowapelekea kutokua salama,”alisema.
Alisema Pemba asili yake ni sehemu salama na sehemu iliyotulia, mwaka jana 2021 idadi ya waliopata maambukizo ilikuwa ni zaidi ya 200 mwaka huu ndio kwanza mwanzo watu 300 ambapo ni ongezeko jipya.
Aliwashauri vijana hao kwenda kupima ili kujua hali za afya zao ziko wapi, sambamba na kujilinda na afya zao kwa lengo la kuepuka maambukizo mapya ya VVU.
Nae Afisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Pemba Ibrahim Saleh Juma, alisema Wizara yake imefarajika sana kuona vijana hao wameitwa na kupatiwa elimu juu ya masuala ya VVU na Ukimwi nchini.
Kwa upande wake Mratib wa Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouka, alisema mwaka 2021 Pemba hali haikuwa nzuri sana watu 211 waliambukizwa VVU, wakati mwaka huu 2022 maambukizi yamepitiliza na kufikia zaidi ya watu 300 wameshaambukizwa.
Alisema kuna maeneo yanaongoza kwa kuwa na tabia hatarishi kwa vijana, ikiowemo Wawi, Vitongoji, Chake Chake, Msingini, huku akiwataka waendesha bodaboda kuwa makini na abiri wanaowapakia.
Aidha alisema athari za maambukizi ya ukimwi ziponyingi, huku akiwataka kujikinga na magonjwa ya kujamiana, pamoja na kuachana kabisa na ngono zembe.
MWISHO