HABARI PICHA: WAZIRI wa Afya Zanzibar ahamasisha matumizi ya kadi za matibabu.
PICHA NO:1. MASHEHA wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na watendaji wa Afya ndani ya Mkoa huo, wakifuatilia kwa makini hutuba ya Waziri wa Afya wakati wa Mkutano wa uhamasishaji wa matumizi ya kadi za matibabu kwa wananchi, mkutano uliofanyika huko Wete na kuandaliwa na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa Phamaccess International Tanzania.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na kuwaonyesha masheha, watoa huduma za afya, wakurugenzi wa halmashauri na mabaraza ya miji na wakuu wa wilaya, kadi za matibabu wakati wa mkutano wakuhamaisha matumizi ya kadi hizo huko Wete na kuandaliwa na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa Phamaccess International Tanzania.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, akizungumza katika mkutano wa uhamaishaji juu ya matumizi ya kadi za matibabu, kwa wananchi wanapokwenda spitali mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa Phamaccess International Tanzania.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)MKURUGENZI Mkaazi wa Phamaccess Intarnational Tanzania Dr.Heri Marwa akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji juu ya matumizi ya kadi za matibabu, kwa masheha, watoa huduma za afya, wakurugenzi wa Halmashauri na mabaraza ya Miji na wakuu wa wilaya, mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa Phamaccess International Tanzania.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBADr.Abdul-latif Khatib Haji kutoka Wizara ya Afya, akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa kadi ya matibabu, kwa masheha, watoa huduma za afya, wakurugenzi wa Halmashauri na mabaraza ya Miji na wakuu wa wilaya, mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa Phamaccess International Tanzania.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)VIONGOZI wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kulia ni katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba Dr.Ali Khatib Bakar, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Wete Dr.Hamad Omar Bakari, wakifuatilia kwa makini mkutano wa uhamasishaji umuhimu wa matumizi ya kadi za matibabu, mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa ufadhili wa Phamaccess International Tanzania.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)