Tanzania yashinda dhidi ya Uzbekistan kwa goli 2-0 kwenye mechi iliyochezwa leo Oktoba 3, 2022 nchini Uturuki.
Kwa matokeo hayo Tanzania inasubiri mchezo kati ya Poland na Hispania utakaochezwa majira ya saa 12:00 jioni, huo ndio mchezo utakaoamua nani kati ya Poland na Tanzania kushika nafasi ya pili katika kundi lao.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania wakishangilia ushindi wao bao 2–0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Uzbekistan mchezo uliofanyika leo Nchini Uturuki Michuano ya Kombe la Dunia kwa Watu wenye ulemavu.