NA ABDI SULEIMAN.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema tayari imeshajipanga vya kutosha, katika kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa wa EBOLA pale utakapotokea nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba hivi karibuni.
Alisema mipango hiyo ni pamoja na kuweka wataalamu katika maeneo yoyte ambayo wananchi wanayatumia kuingia nchini, ikiwemo viwanja vya Ndege, Bandarini hata katika bandari bubu zilizomo ndani ya Zanzibar.
Waziri alisema timu ya wataalamu wa afya wapo kuangalia kila anayeingia nchini kutoka nje ya nchini, kuhakikisha wanapimwa na kama atagundulika kuwa na dalili basi atapelekwa katika maeneo husika kwa ajili ya kutenga na kupatiw amatibabu.
“Ebola imeingia nchini Uganda, Tanzania bado maradhi haya hayajaingia, Mungu atuepushie mabali lakini ukisikia mwenzako ananyolewa wewe utie maji, tayari tupo kikamilifu pale tu mgonjwa atakapobainika basi maeneo yapo ya kumuweka na kumpatia huduma,”alisema.
Akizunguzmia juu ya suala la Vifaa Tiba, alisema vifaa vifaa vimeshatayarishwa, wafanyakazi wameshapewa mafunzo, hata sehemu za kuwazika ili kuona maradhi hayo hayaenei nchini.
Aidha alisema Serikali iko macho na kuona maradhi hayo hayaingi nchini, kupitia katika mipaka yake kwani ulinzi umeimarika katika maeneo yote kwa mgeni yoyote atakaeingia.
Kwa upande wa Chanjo ya Surua, aliwataka wananchi kuhakikisha wanawafikisha watoto wao katika vituo vya afya kwa lengo la kupatiwa chanjo hiyo, kwani watu 10 wameshafariki kwa ugonjwa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ndani wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Pemba Khamis Arazak Khamis, alisema tayari wameshafanya vikao vitatu na timu yao ya wataalamu, kujalia juu ya ugonjwa huo pale tukio litakapotokea ikiwemo sehemu ya kupelekea kumtenga na kupatiwa matibabu.
“Sisi kamisheni lazima tushirikiane na wataalamu wa wizara ya afya na kila kitu kipo sawa, ikiwemo suala la kujikinga, kujiandaa, suala la kukabiliana nalo na kufanya tathmini”alisema.
Akizunguzmzia juu ya mijikinga na kujiandaa, alisema tayari wameshandaa mikakati na sekta husika, kuyataka maeneo ya kuingilia ikiwemo viwanja vya ndege na barandarini, kupimwa wananchi wote wanaoingia.
Aidha alisema tayari wametenga neo la chuo cha mafunzo ya Amali Vitongoji kwa Pemba, kuwa ndio sehemu pekee pa kuhifadhiwa wagonjwa watakaobainika na kupatia matibabu.
Hata hivyo aliwataka wananachi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo, kwani wanapaswa kutokupuuzia pale dalili zitakapoanza kujitokea.
MWISHO