Mamlaka nchini Tanzania inaendelea kukabiliana na moto mkali katika mlima Kilimanjaro kwa siku ya pili.
Moto huo ulianza usiku wa kuamkia leo katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro kutokana na moshi mkubwa.
Zaidi ya wazima moto 500 wako kwenye tukio
Zaidi ya wazima moto 500 wapo eneo hilo tangu jana (Jumamosi) kusaidia kuzima moto huo uliokuwa ukiwaka.
Hata hivyo, chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Pia, hakuna kifo au majeruhi wameripotiwa kufikia sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu alisema jana jioni walichukua ndege kwenda kufanya tathmini ya uharibifu huo, lakini walilazimika kuondoka eneo hilo baada ya kujaribu zaidi ya mara mbili na kushindwa.
‘’Tumezunguka eneo hilo zaidi ya mara mbili, lakini hatukuweza kufika eneo la moto kwa sababu moshi ulikuwa mkubwa, tuliamua kurudi na hali inapokuwa shwari, tutarudi,’’ alisema Bw Nurdin.
Aidha, mashuhuda katika eneo hilo walisema hewa nzito ya moshi na miali mikubwa ya moto inaonekana.
Mwisho wa Twitter ujumbe
Sio mara ya kwanza kwa moto kutokea Mlima Kilimanjaro
Hii si mara ya kwanza moto kutokea kwenye maeneo ya Mlima Kilimanjaro.
Mnamo 2020, tukio la moto liliharibu mamia ya mimea kwenye kilele cha juu zaidi barani Afrika.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo Hamisi Kigwangalla alieleza kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa upepo, nyasi kavu na vichaka vimekuwa changamoto kubwa na kuwa wataanza kutumia ndege na helikopta na ndege katika shughuli za kuzima moto huo.
Tanapa ilieleza kuwa ukaguzi wa helikopta ulibainisha kuwa eneo kubwa lililoathirika na moto lilikuwa limedhibitiwa na kuwa maafisa kutoka idara ya zimamoto na Tanapa walifika katika meneo yote ambayo yaliathirika ili kudhibiti moto huo.
Taarifa ya Tanapa wakati huo ilibainisha kuwa, moto huo uliathiri eneo la kilomita 95.5 sawa na asilimia 5 la hifadhi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1700.
CHANZO CHA HABARI BBC NEWS SWAHILI