Friday, January 31

WANAFUNZI Elfu 20,904 wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya darasa la nne leo.

NA ABDI SULEIMAN.

WANAFUNZI Elfu 20,904 wanatarajiwa kuanza kufanya mitihani yao ya darasa la nne leo Oktoba 24 mwaka huu Kisiwani Pemba, ambapo mwaka huu itakuw achini ya kamati za kitaifa za mikoa badala ya Wizara.

Mitihani hiyo inayofanyika nchi nzima, kwa upande wa Pemba maandalizi yote yameshakamilika ili kuona mitihani inafanyika kwa salama na amani.

Hayo yameelezwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mohamed Nassor Salim, wakati alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizo huko ofisini kwake Mjini Chake Chake.

“Mwaka huu 2022 wanafunzi 20,904 kwa mikoa miwili ya Pemba, ndio watahiniwa halali waliosajiliwa, kila kitu kiposawa katika mitihani hii,”alisema.

Aidha aliwataka wazazi kuwasaidia kuwaanda watoto, kwa kuwaamsha mapema na kuwapatia chai kulingana na hali za maisha, kwani wanafunzi wengi wanaofanya mitihani ni wadogo sana na mitahani inachuka muda mrefu madarasana, hivyo watawapunguzia usumbufu wa kufikiria kula.

“Watakapokua madarasani wasiweze kusumbuka, watoto hao ni wadogo na mitihani inachukua muda mrefu, kipindi cha mitihani skuli vyakula vinakua mbali, kipindi cha mapumziko watoto wanachukua muda mrefu kwenda kutafuta kula na kuacha kupitia mabuku yao tena”aliongeza.

Akizungumzia suala la maandalizi ya mitihani, alisema ni mazuri kwani tayari wameshajiandaa vizuri na wameshapatiwa miongozo yote na mafunzo kwa walimu wote watakaosimia mitihani hiyo, na kuona hakuna udanganyifu wala hujuma itakayotokea.

Alisema wizara kazi yake ni kutoa fedha na tayari wameshakamilisha katika kuziwezesha kamati ikiwemo sehemu ya kuhifadhiwa mitihani, wala hakuna shida ya miundombinu yoyote  kwani madarasa mapya yameruhusiwa kutumika katika mitihani hii na wanafunzi hawatakaa katika madarasa mabovu au yanayovuja.

Hata hivyo alisema mitihani itaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni, huku akiwataka watu wasio husika kuwa mbali na vituo vya mitihani, kwani vikosi vya ulinzi na usalama vitakua macho na yoyote atakaehujumu ataadhibiwa.

Kwa upande wa watoto wenye mahitaji maalumu, alisema Wizara imetumia zaidi ya milioni tatu, katika kutengeneza nukta nundu ili kuwasaidia wanafunzi wasio ona.

Alisema baadhi ya wanafunzi wataengezewa muda wa ufanyaji wa mitihani kwa wenye mahitaji maalumu, pia kuna mitihani maalumu kwa wanafunzi hao, sambamba na uwepo wa wataalamu mbali mbal;I ambao wataweza kuwasaidia pale watakapokuwa na mataatizo.

MWISHO