Monday, March 3

Tetesi za soka ulaya Jumanne 25.10.2022

Tottenham inataka kukubaliana kuhusu kandarasi mpya na mshambuliaji wa England Harry Kane mapema mwaka ujao na wana uhakika mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ataweka mustakabali wake wa muda mrefu katika klabu hiyo. (90Min)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic anasema klabu hiyo ya Bundesliga, ambayo imekuwa ikihusishwa na kutaka kumnunua Kane, haitaingia sokoni katika dirisha la uhamisho la Januari. (Bild, via Christian Falk)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag angependa kumbakisha mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo hadi mwisho wa msimu huu, hata hivyo ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 hatakubali hali ya kucheza mara chache basi ataruhusiwa kutafuta klabu mpya. (Usajili unahitajika)

Ronaldo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambulizi wa Bayer Leverkusen wa Jamhuri ya Czech Patrik Schick, 26, mchezaji wa kimataifa wa Canada wa Lille Jonathan David, 22, na Mfaransa wa Lyon Moussa Dembele, 26 ndio chaguo linalopendekezwa na Ten Hag kuchukua nafasi ya Ronaldo. (Mirror)

Ronaldo yuko tayari kurejea Italia, huku Napoli wakiwa bado wana nia ya kukamilisha mpango huo waliokuwa nao tangu msimu wa joto. (Sun)

Chelsea itaweka kipaumbele kwa kumnunua mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, badala ya kumnunua Ronaldo. (CBS, kupitia Mirror)

Rafa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Rafael leao

Paris St-Germain wana shaka juu ya uwezo wao wa kuendelea kulipa kandarasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 una thamani ya £549m kwa miaka mitatu – robo ya jumla ya bajeti ya timu. (Sport)

PSG wamekanusha kuhusu takwimu hizo. (Fabrizio Romano)

Chelsea wanafikiria chaguo kumtoa kwa mkopo kwa mlinda mlango Mmarekani mwenye umri wa miaka 18 Gabriel Slonina, ambaye walimsajili kwa £12m msimu wa joto. (Evening Standard)

The Blues bado wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Urusi Arsen Zakharyan, 19, kutoka Dynamo Moscow. (Sport Express, kupitia Metro)

Antonio Conte anaamini atahitaji madirisha matatu zaidi ya uhamisho ili kuboresha upana wa kikosi cha Tottenham. (Times)

Spurs

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Nyota wa Spurs

Real Madrid wanajiandaa kumpa mkataba ulioboreshwa wa miaka mitatu mshambuliaji wa Uhispania Marco Asensio, 26, ambaye alihusishwa na kuhamia Arsenal, Liverpool na Tottenham baada ya kukataa ofa ya awali. (Ser Deportivos)

Mkufunzi wa Celtic Ange Postecoglou amepuuzilia mbali uvumi wa kutaka kuhamia Ligi kuu England, huku kukiwa na ripoti zinazomhusisha na kazi katika klabu za Brighton na Leicester City. (Mail)

Liverpool watachuana na Manchester United kwa ajili ya kumsajili beki wa kati wa Benfica Mreno Antonio Silva, 18. (O Jogo, via Team Talk)

CHANZO CHA HABARI BBC NEWS SWAHILI


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1741001051): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48