Monday, March 3

UJIO WA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASI YA KONGO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mhe.Felix Tshisekedi katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar katika mazungumzo yao waligusia ushirikiano baina nchi mbili hizo ikiwemo Uchumi na Biashara.[Picha na Ikulu]
Ali Mwinyi amekutana  na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi katika mazungumzo mafupi yaliofanyika Ikulu Zanzibar, mwishoni mwa wiki iliopita.

 

Katika mazungumzo hayo Marais hao walijadili umuhimu wa kuangalia maeneo zaidi ya ushirikiano  kati ya nchi mbili hizo kupitia sekta za kiuchumi na Biashara, wakati huu biashara ya usafirishaji wa Dagaa kutoka Zanzibar kwenda nchini Kongo ikishamiri.

 

Rais Dk. Mwinyi alimuomba Rais Tshisekedi kuutangaza Utalii wa Zanzibar kwa wadau wa sekta ya Utalii nchini Kongo.

 

Aidha, Rais Tshisekedi alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi kwa mapokezi mazuri aliyopata yeye na ujumbe aliofuatana nao na akatumia fursa hiyo kuahidi kuongeza ushirikiano kati nchi mbili hizo kwa maslahi ya mataifa hayo na wananchi wake.

 

Rais Tsisekedi alizuru Tanzania kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili, ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

 

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.