Friday, February 28

PENATI YA UTATA YAING’ARISHA YANGA UGENINI

Penati ya utata ya Yanga iliyolalamikiwa sana na wachezaji wa Geita Gold kutokana na Mchezaji wa timu hiyo kuunawa mpira akiwa nje ya 18 na mwamuzi kushindwa kutafsiri vizuri sheria Katika tukio Hilo  kumewafanya mabingwa hao  wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa (Unbeaten) katika mechi 45 za ligi baada ya  kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Shujaa wa Yanga ni Winga mtukutu Bernard Morrison aliipatia bao timu yake mnamo dakika ya 45  kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Geita kuunawa Mpira ndani ya 18.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 20 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.

Mchezo mwingine umepigiwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Tanzania Prisons imenusurika kufungwa na Namungo FC baada kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1