Saturday, March 15

YANGA SC YASHINDWA KUTAMBA KWENYE UWANJA WAKE WA NYUMBANI DHIDI YA CLUB AFRICAIN

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na timu Club African kwenye michuano ya kufuzu makundi kombe la shirikisho .

Yanga Sc licha ya kulazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo huo wameonesha kuhitaji ushindi kwa kucheza kandanda safi kwa kujitahidi kutafuta bao bila mafanikio .

Yanga Sc inahitaji sare yoyote ya mabao kwenye mchezo unaofuata ambao utapigwa nchini Tunisia ili aweze kufuzu hatua ya makundi.