Sunday, March 16

YANGA SC YAPANDA KILELENI, YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0

NA EMMANUEL MBATILO

FISTON Kalala Mayele amendelea kutikisa nyavu ndani ya ligi kuu NBC baada ya leo kupachika mbao mawili na kuisaidia timu yake kuondoka  na ushindi wa mabao mawili dhidi ya Dodoma Jiji.

Mchezo  huo ambao ulichezwa kwenye dimba la Liti  mkoani Singida tumeshuhudia wachezaji wengi wa Yanga kupata majeruhi  kwenye mchezo huo akiwemo nahodha wao Bakari Nondo Mamnyeto na Feisal Salum.

Kipindi cha kwanza Yanga Sc ilikuwa mbele  kwa bao 1-0, bao ambalo lilifungwa kabla  ya kwenda mapumziko  dakika ya 43 ya mchezo.