Thursday, January 16

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 29.11.2022

Christopher Nkunku

Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 25, kutoka RB Leipzig kwa mkataba wa muda mrefu, ambao una thamani ya zaidi ya euro 60m. (Fabrizio Romano)

Mshambulizi wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35, hajakubali dili la kujiunga na Inter Miami licha ya ripoti kupendekeza kwamba anakaribia kufanya hivyo. (ESPN)

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Jordan Henderson

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Caglar Soyuncu (kulia) alicheza dhidi ya Latvia katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia

Roma wanafikiria kumnunua mlinzi wa Leicester City na Uturuki Caglar Soyuncu, 26, mwezi Januari. (Calciomercato – in Italian)

Chelsea haiko tayari kumruhusu winga wa Marekani Christian Pulisic kuondoka kwa mkataba wa mkopo msimu huu wa baridi na wangependelea uhamisho wa kudumu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail)

Brighton wameanza mazungumzo na Molde ya Norway ili kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 19. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Uingereza Gareth Southgate anatazamiwa kuwaita tena Jordan Henderson na Kyle Walker kwenye kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa makundi wa Kombe la Dunia la Three Lions dhidi ya Wales siku ya Jumanne. (Times – subscription required)

Bayern Munich wanaamini kuwa wamekamilisha makubaliano ya kumsaini kiungo wa kati wa RB Leipzig na Austria Konrad Laimer, 25. (90min)

Cameron Archer

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Sunderland ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Ubingwa vinavyomwinda mshambuliaji wa Aston Villa Muingereza Cameron Archer, 20, mwezi Januari. (Football Insider)

Manchester United wako tayari kuwarejesha kwenye orodha ya wachezaji waliotolewa kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari, akiwemo beki wa kulia wa Uingereza Ethan Laird, 21, katika QPR, kiungo wa kati wa Tunisia mwenye umri wa miaka 19 Hannibal Mejbri kutoka Birmingham City na winga wa Ivory Coast Amad. Diallo, 20, kutoka Sunderland. (Manchester Evening News)

CHANZO CHA HABARI BBC NEWS SWAHILI.