Wednesday, January 15

Kuhamasisha utumiaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni na wenyeji kutasaidia kufanikisha mpango mkakati wa kitaifa wa kukuza na kuendeleza kiswahili nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab akiwahutubia wakufunzi waliyofika katika mafunzo ya Kiswahili kwa wageni  mara baada ya kuwasili  ukumbi wa Sanaa Mwanakwerekwe  mjini Zanzibar.

Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili (BAKIZA) Dkt. Mwanahija Ali Juma akimkaribisha mgeni rasmin  wakati alipowasili katika mafunzo ya Kiswahili kwa wageni yaliyoandaliwa na baraza la kiwsahli huko ukumbi wa Mwanakwerekwe Mijini Zanzibar. (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab (kushoto) Kamishina Idara ya Utamaduni Dkt. Omar Salum Mohammed.

Daktari wa mashairi kutoka chakuwaza Issa Ali Issa akitumbuiza ushairi mara baada ya kuwasili mgeni rasmin katika mafunzo ya Kiswahili kwa wageni huko ukumbi wa Sanaa mwanakwerekwe mjini Zanzibar.

Mmoja ya washiriki waliyofika katika mafunzo ya Kiswahili kwa wageni  akichangia mada  marabaada ya kupatiwa mafunzo hayo huko ukumbi wa Baraza la Sanaa Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.

                       Picha na Miza Othman- Maelezo Zanzibar.

Na Khadija Khamis Maelezo 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana. Utamaduni na Michezo, Fatma        Hamad Rashid amesema kuhamasisha utumiaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni na wenyeji kutasaidia kufanikisha mpango mkakati wa kitaifa wa kukuza na kuendeleza kiswahili nchini

Hayo ameyasema katika ukumbi wa Baraza la Kiswahili Zanzibar ( BAKIZA ) Mwanakwerekwe,Wilaya ya Magharibi ‘B’ wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya  ufundishaji wa kiswahili kwa wageni.

Amesema Serikali tayari imeshafungua milango kwa wageni hivyo Iko haja ya kujua njia Bora ya ufundishaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni jambo ambalo litatoa fursa ya  kuuendeleza Utamaduni huo kwa ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema Zanzibar kuna wataalamu wazuri wa ufundishaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni jambo ambalo litasaidia kukirithisha kiswahili kutoka kizazi na kizazi pamoja na kukisomesha kwa wageni .

Alifahamisha kuwa kuna kila ya sababu ya kujivunia kutokana na umahiri  mbinu na ustadi wa wakufunzi hao kwa njia bora wanazozitumia kwa  wanafunzi wao.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar Dkt Saade Said Mbarouk amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu kuwa na njia bora ya ufundishaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni na wazawa.

Mafunzo hayo ni ya mara ya kwanza kufanyika hapa Zanzibar  na yanatarajiwa kuwa endelevu ili kuhamasisha na kuendeleza utamaduni wa lugha ya kiswahili  kwa wageni.