NA ABDI SULEIMAN
VIJANA Kisiwani Pemba wametakiwa kufahamu kwamba suala la amani lina umuhimu wake katika kuleta maendeleo nchini, hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha amani ilyopo nchini wanaiyendeleza kwa maslahi ya taifa.
Alisema amani ni hazina pekee ambayo baadhi ya matifa duniani wanaitafuta, hivyo vijana wanapaswa kuilinda kwa hali yoyote amani hiyo.
Hayo yameelezwa na mratibu wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Pemba Ali Mussa Bakar, wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku mbili kwa vijana kutoka Wilaya ya Wete, kupitia mradi wa AMANI VISIWANI unaotekelezwa na CYD kwa ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeloe Duniani (UNDP).
Aidha alifahamisha kwamba uwepo wa amani unapelekea upatikanaji wa huduma bora, zipo nchi hazina anami na maendeleo hakuna ni machafuko kila siku.
“Amani ni muhimu katika kuleta maendeleo, vijana kuhakikisha wanakua mabalozi kwa wenzo ili vijana wengizaidi waweze kufikiwa na elimu hii ya amani Visiwani,”alisema.
Hata hivyo Mratib huyo, alisema suala la amani sio mpaka kuwe na machafuko, bali ni kuwajenga vijana katika mustakbali mzuri wa kuona wanadumisha na kushiriki katika maendeleo endelevu ambayo serikali inayataka.
Hata hivyo alisema huwezi kumuendeleza kijana kiuchumi au michezo kama hakuna amani, dhana hii ni muhimu sana katika mikakati ya serikali ya awamu ya nane, ambayo imedhamiria kubadilisha maisha ya vijana wa Zanzibar.
Mapema mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya CYD Zanzibar Hashim Pondeza, alisema Mradi wa AMANI VISIWANI una malengo matatu moja ni kuwawezesha vijana kwa kuwapa uwelewa kuhusu masuala mazima ya ulinzi Amani na Usalama, kwani vijana wanafanya mambo mengi lazima wapatie limu hiyo.
“Serikali imeona ipo haja ya kuzungumzia waziwazi juu ya masuala ya ulinzi Amani na Usalama, vizuri sote tukawa walinzi na waumini wa kulinda Amani itiyopo,”alisema.
Alisema lengo jengine ni kutoa fursa kwa wadau wengine kuweza kukaa pamoja kuzungumza jinsi gani vijana wanamchango katika suala la ulinzi wa amani.
Aidha alisema vijana wananafasi kubwa ya kuendeleza amani ya Zanzibar, huku akiwataka vijana kuhakikisha wanaitunza na kuithamini amani iliyopo nchini.
Nae Mkufunzi wa Mafunzo hayo, ambae ni mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Taifa SUZ Dk.Said Mohd Khamis, alisema suala la amani ni muhimu katika nchi yoyote duniani, hivyo vijana wanapaswa kuitunza na kuithamini amani hiyo.
Alisema msingi wa ujenzi wa amani na Usalama ni kwa watu wote, kwani unajenga usalama wa kiuchumi na kijamii unaojikita katika maendeleo endelevu.
“Hakuna maendeleo yoyote duniani bila ya kuwepo kwa amani na utulivu, hakuna amani na utulivu bila ya kuwepo utawala wa sheria,”alisema.
Kwa upande wake Ibrahim Mjaka Mussa kutoka Wete, alisema Viongozi wa dini wana mchango mkubwa wa kuelimisha jamii, juu ya suala la amani ni vizuri kushirikiana.
Alisema viongozi wa vyama vya siasa wanapaswa kuwapatia elimu wafuasi wao, sambamba na kuingiza suala la amani katika mitaala ya elimu na kufundishwa kuanzia ngazi za msingi maskulini.
Naye Zamzam Ali Juma, alisema vijana wenyewe wanamchango mkubwa wakushajihishana, ili kutumia vigenge vyao na vibaraza kuhubiri suala la amani kwa wenzao.
Jumla ya Vijana 40 kutoka wilaya ya Wete, wameshiriki mafunzo Vijana Amani Maendeleo kupitia mradi wa AMANI VISIWANI unaotekelezwa na Kituo cha Majadiliano kwa Vijana Zanzibare (CYD) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Umaja wa Mataifa UNDP.
MWISHO