NA MARYAM HAMAD
Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wameaswa kufuata maadili ya uandishi wa habari na kufanya kazi zao kwa weledi na kujiepusha kusambaza maudhui yenye kusababisha uchochezi wanapotumia mitandao ya kijamii.
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti Mstaafu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba PPC Said Moh’d Ali alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano mkuu maalumu ulioandaliwa na Klabu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba Chachani Chake Chake.
Amesema iwapo waandishi watafuata maadili na kutumia taaluma yao ipasavyo kutaepusha migogoro katika jamii ambayo inaweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu hiyo Bakar Mussa Juma Amewataka waandishi wa habari ambao hawajawa wanachama kujiunga na Klabu hiyo ili kuwasogeza karibu na wenzao.
Akisoma maazimio ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC uliofanyika hivi karibuni Msaidizi katibu mkuu wa PPC Mchanga Harroub Shehe amewasilisha maadhimiyo hayo ambayo yanahitaji kujadiliwa na kila klab nchini.
Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo mkuu maalum wakapata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo yao.
Mkutano huo pamoja na kujadili maazimio hayo pia uliweza kuwajadili wanachama wapya saba na kuridhia maombi yao na kuwagawa vitendea kazi kwa vyombo vya habari kutoka UTPC.
KUANGALIA HABARI HII BOFYA VIDEO HAPO CHINI