Monday, November 25

WAJUMBE WAPITISHA MRADI WA UJENZI WA MABANDA 4 YA SKULI YA MSINGI WAWI KUPITIA MFUKO WA JIMBO.

MWENYEKITI wa Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, ambae pia ni Mwakilishi wa jimbo hilo Bakar Hamad Bakar akiongoza kikao cha kamati ya mfuko wa jimbo kikao hicho kilichofanyika mjini Chake Chake
WAJUMBE wa Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Wawi wakimsikilisha mwenyekiti wa kamati hiyo mwakilishi wa jimbo hilo Bakar Hamada Bakar, wakati wakupitisha mradi wa maendeleo utakotekelezwa 2023 ndani ya jimbo hilo, kikao kilichofanyika mjini Chake Chake.
DIWANI wa Wadi ya Kobokoni Vitongozi Ali Yussuf Juma, akizungumza wakati wakikao cha kamati ya maendeleo ya Jimbo la Wawi, iliyokutana chini ya mwenyekiti wake Mwakilishi wajimbo hilo na kupitisha mradi wa ujenzi wa skuli kwa mwaka 2023

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

NA ABDI SULEIMAN.

WAJUMBE wa kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, wamepitisha mradi wa ujenzi wa mabanda manne ya skuli ya msingi Wawi kupitia mfuko wajimbo hilo.

Mradi huo ulianza mwaka 2022 kwa kujengwa fondesheni, baada ya kumalizika kwa skuli ya Msingi na maandalizi Kibokoni Vitongoji na mwaka 2023 mradi huo unatakiwa kuendelezwa ili uweze kukamilika.

Kikao cha kupitisha mradi huo, kiliongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Mwakilishi wa jimbo la Wawi Bakar Hamad Bakar, na kufanyika katika ukumbi wa baraza la mji Chake Chake.

Akizungumza katika kikao hicho mwakilishi huyo, alisema mfuko huo unapata Milioni 20 kila mwaka, kwama 2022 walijenga na kumaliza skuli ya kibokoni pamoja na ujenzi wa vyoo kwa skuli hiyo.

“Tatizo kabla ya kutekeleza mradi mwengine kwanza tunapaswa kumaliza mradi uliopo, sasa na sisi wajumbe tuhakikishe mradi huu uliopo unamalizika,”alisema.

Alisema tayari jengo hilo hadi kukamilika kwake inatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 32, hadi tufali za juu na litakapobakia kukabidhiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Hata hivyo alisema katika utekelezaji wa mradi huo, hakutokua na fedha yoyote itakayotumika vibaya wala kutokea upotevu wake kwani atahakikisha nafuatilia kila hatua.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema tayari miradi mbali mbali imetekelezwa katika jimbo hilo la Wawi, ikiwemo ujenzi wa barabara, ukarabati wa madarasa ya skuli, ujenzi wa maskani za CCM na kusaidia mipira ya maji.

Wakichangia katika mkutano huo, wajumbe wa kamati hiyo wamepitisha ujenzi wa skuli hiyo huku wakisisitiza kuendelea kuwa wamoja na kutimiza malengo ya kamati hiyo kikamilifu katika kuhudumia jamii.

Wamesema watahakikisha kila mradi unaopitishwa unatekelezwa ipasavyo na kukamilika kwa wakati, ili wananchi waendelee kuwa na imani na mwakilishi oa.

Kwa upande wao wageni waalikwa katika mkutano huo, waliwataka wajumbe wakakamti hiyo kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika utekelezaji wa miradi yote iliyomo ndani ya jimbo hilo, sambamna kuwa wawazi katika matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo.

MWISHO