Picha na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.
Na Rahma Khamis Maelezo- Zanzibar
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh, Mgeni Hassan Juma amewataka Wajumbe wa Baraza hilo kuwa makini ,wasikivu kwa kutoa maoni yao ili kuifamu Sheria mpya ya uvuvi na Uchumi wa Buluu inayotarajiwa kutumika mara baada ya wajumbe kuipitisha.
Akifingua semina kwa wajumbe wa Baraza hilo kuhusu uwelewa wa rasilimali ya sheria mpya za Uvuvi na Uchumi wa Buluu katika Hoteli ya Verde Mtoni amesema kuwa kuwa semina hiyo ni muhimu kwani itawapa uwelewa wajumbe kuifahamu sheria kwa lengo la kuimarisha Sekta ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu Ili kufika malengo.
Amefahamisha kuwa kufanya hivyo ni vyema kwani itatoa fursa Kwa wajumbe kuweza kuwasilisha maoni yao ili iweze kutumika Kwa wavuvi na kuinua Uchumi wa Zanzibar.
Nae Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mh,Suleiman Masoud Makame amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kutoa nafasi kwa wajumbe kuweza kuijadili ili ianze kutumike
Aidha amefahamisha kuwa kuundwa kwa sheria hiyo ni hatua kubwa ya kimaendeleo kwani itawasaidia wavuvi na wakulima wa baharini kuweza kunufaika
Amefafanua kuwa katika kutengeneza sheria hiyo awali walichukua maoni kutoka Kwa wavuvi Ili kujua matatizo wanayowakabiliana nayo Ili kuweza kutatua changamoto hizo.
Kwa upande wake Muwakilishi kutoka UNDP ambae pia ni Mshauri wa kiuchumi Dkt Onamuli amefahamisha kuwa wameamua kushirikiana Serikali ya Zanzibar katika sekta ya Uchumi wa Buluu Ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza dhana ya Uchumi wa Buluu.
Aidha amefahamisha kuwa katika kuendeleza dhana hiyo wameweza kusaidia kutengeneza sera za Uvuvi na sheria ya Uchumi wa Buluu Ili kusaidia mpango mkakati wa Serekali ya Zanzibar.
Katika semina hiyo madatatu zimejadiliwa ikiwemo Uwasilishwaji wa utangulizi wa sharia na Sera ya uvuvi, Uwasilishwaji wa muhtasar wa sheria ya uvuvi, na Sheria ya uhifadhi na Sheria ya utafiti.