Thursday, January 16

HABARI PICHA: Uwekaji wa jiwe la msingi kituo Cha afya na mahanga ya kulala askari huko katika Kambi ya KM KM Gando.

WAZIRI wa ardhi nyumba makaazi na maendeleo Rahma Kassim Ali akizungumza na wananchi wa Gando wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha afya na mahanga ya kulala askari huko katika Kambi ya KM KM Gando Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisho ya kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahfoudh akitoa maelezo juu ya mradi wa ujenzi wa Kituo Cha afya na mahanga ya kulala askari katika kituo Cha KM KM Gando Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisho ya kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
MKUU wa Kamandi KM KM Pemba Mussa akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha afya na mahanga ya kulala askari katika kituo Cha KM KM Gando Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisho ya kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
WAZIRI wa ardhi nyumba na makaazi na maendeleo Rahma Kassim Ali akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha afya KM KM Gando Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisho kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha afya na mahanga ya kulala askari katika kituo Cha KM KM Gando Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisho ya kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
VIJANA kutoka Wilaya ya Micheweni wakiimba wimbo Maalum wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha afya KM KM Gando Wilaya ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisho ya kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

(PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)