Thursday, January 16

KAMATI YA TFF YAMIWTA FEISAL KUJIBU SHUTUMA ZA YANGA

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemuita kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kujibu malalamiko ya klabu yake, Yanga.

Yanga imetuma malalamiko TFF kufuatia Feisal kushinikiza kuvunja mkataba na kujitoa kwenye timu hiyo na kwa sasa tayari yuko Dubai akifanya mazoezi binafsi.