Wednesday, January 15

Lishe bora lina mchango mkubwa katika mwili , jamii imetakiwa kutumia vyakula vya matunda na mboga mboga ili kuweza kuwa na afya imara

Na Shaib Kifaya Pemba .                         

Jamii  imetakiwa kutumia vyakula  vya matunda na mboga mboga ili kuweza kupata lishe   bora na afya njema  ambayo itaweza kujikinga na maradhi mbali mbali.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mwalim Khamis Abdalla Said , huko skuli ya sekonday Madungu Chake chake wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya lishe bora kwa waalimu wa Skuli Mbali Mbali Kisiwani Pemba.

Alisema  suala la lishe bora lina mchango mkubwa katika mwili na kumfanya mtoto mwenye lishe bora kuwa na ufahamu mzuri katika masomo yake .

Akiwasilisha mada katika mafunzo  hayo  Mkufunzi kutoka Kitengo cha Elimu Mjumuisho Halima Mohamed Khamisi amesema mtoto anayekosa lishe bora hupelekea kukosa kinga katika mwili wake.

Alifahamisha watoto wenye umri wa kwenda skuli wenye makundi kuanzia umri wa miaka 4hadi 19 kwa utaratibu wa kwenda skuli Zanzibar ambapo nikipindi cha ukuwaji endelevu wa mwili wake wa kihemko wa hisia .

Aidha alisema ukosefu wa lishe na magonjwa kwa umri huo nitatizo na kupelekea athari za muda mrefu na kupelekea maambukizi ya vimelea ambapo huenea Zaidi na kuongezeka upungufu wa madini joto .

Nae mwalimu Abdalla Khamis Hamad kutoka skuli ya Fidel Kasro ,alisema mafunzo  ya lishe bora kwa wanafunzi yatawasaidia watakapo kuwa skuli hata majumbani kwao kwani wataweza kutambua matumizi sahihi ya utumiaji wa vyakula bora ambavyo vinahitajika kutumia na kipi ambacho hakihitaji kiaweza kuleta madhara kwao.

Kwa  upande wake mwalimu Khadija Abass Ali ,amesema katika Mafunzo hayo wamejifunza mambo mbali mbali ikiwemo kujua athari za ukosefu wa afya bora na kutoa elimu kwa jamii na familia zao kutumia vyakula vya matunda na mboga mboga kwa kuimarisha afya zao na kuacha ulaji holela wa vitu ambavyo vinachangia kupelekea madhara ya afya zao ..