KHADIJA KOMBO-PEMBA
Zaidi ya wagonjwa mia moja (100) wakiwemo wanaume 54 na wanawake 47 wanaosumbuliwa na magonjwa ya mtoto wa jicho wamefanyiwa upasuaji katika kambi maalum za matibabu ya macho huko Hospitali ya Wete na Abdalla mzee Mkoani Kisiwani Pemba.
Akizungumza na wagonjwa hao mara baada ya kufanyiwa upasuaji Daktari bingwa wa magonjwa hayo Dr. Njau Sekondri amesema miongoni mwa njia za kuepuka magonjwa hayo ni kuzingatia mlo kamili ili kujenga afya ili kuepuka maradhi nyemelezi.
Kw upande wake Mratibu wa huduma za macho Zanzibar Dr. Fatma Juma Omar amewataka wagonjwa hao kuepuka kufanya kazi ngumu katika kipindi hiki cha matibabu huku wakipata muda mwingi wa mapumziko ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
Nao wananchi hao wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushiorikiana na wafadhili mbali mbali na kuweza kuwapatia matibabu hayo bila ya gharama yoyote.
KUANGALIA VIDEO YA HABARI HII BOFYA HAPO CHINI