Thursday, January 16

NMB YAKABIDHI VIFAA TIBA KWA RAIS.DK MWINYI.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, akipokea vifaa mbali mbali vya hospitali hiyo kutoka kwa Meneja Mkuu wa Biashara za NMB Zanzibar Naima Said Shaame, wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

LENGO NI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI, KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

NA ABDI SULEIMAN.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru Benk ya NMB kwa kuendelea kuiyunga mkono serikali, katika kusaidia vifaa kwa hospitali ya Wilaya ya Micheweni.

Alisema NMB imekua ikijitahidia kusaidia jamii katika vitu mbali mbali, jambo ambalo linapaswa kuigwa na taasisi nyengine za kifedha nchini.

Rais Dk. Miwnyi aliyaeleza hayo wakati akipokea vifaa mbali mbali kwa hospitali ya Wilaya ya Micheweni, kutoka kwa watendaji wa benk hiyo ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar, iliyoambatana na ufunguzi wa hospitali ya Wilaya hiyo.

Aidha aliwataka watoa huduma za afya kujitahidi kuvutia vifaa hivyo kwa uwangalifu, ili viweze kudumu kwa muda mrefu na viweze kutoa tija.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Biashara za NMB Zanzibar Naima Said Shaame, alisema NMB imekabidhi vifaa kadhaa kwa kusaidia afya za wananchi wanaopata huduma katika hospitali hiyo.

Alisema NMB wana asilimia moja ambayo wanatenga kila mwaka, kwa ajili ya kurudisha kwa jamii, na vipaombele vyao ni Afya na Elimu pamoja na kuangalia na majanga.

Aidha alisema mchango wa benki hiyo, unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu, tayari miradi mbali mbali imekua ikifunguliwa.

“Tumelazimika kutoa hivi leo kama kipaombele chetu kama benk, katika kusaidia jamii na hawa tunaopatiwa huduma ni wateja wetu leo na kesho, hili ni jambo zuri na lakuvutia kwetu sisi benk,”alisema.

Alivitaja vifaa walivyokabidhi ni pamoja na mashuka 200, vitenganisha wodi 10, viti venye magurudumu vitano, mashine tatu za kupimia presha vifaa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 9.

Aidha alisema lengo la NMB ni kuhakikisha wateja wao wanahudumiwa katika mazingira mzuri, kwa sababu mteja mwenye afya ndio mteja mzuri kwa benk.

Aliwataka watnoa huduma za afya katika hospitali hiyo, kuhakikisha vifaa hivyo wanavitunza na kuvithamini ili viweze kuendelea kudumu kwa muda mrefu.

“Sisi kama Benki ya NMB, tunaamini watu wenye afya njema wana tija na wanaweza kushiriki katika mchakato wa kujenga taifa lenye afya bora, Benki kwa miaka saba iliyopita imekuwa ikishughulikia baadhi ya vifaa muhimu vya matibabu na ukarabati wa miundombinu kutoka kwa hospitali mbalimbali nchi, ili kuboresha afya za wagonjwa,”alisema.

Naye meneja wa NMB Tawi la Pemba Hamad Msafiri, aliwataka wananchi kuendelea kujenga imani na benk ya NMB kwa kufungua akaunt na kupatiwa huduma mbali mbali.

Alisema NMB imekua mstari wambele katika kusaidia jamii, kile wanachokipata na Pemba tayari imeshasaidia vitu mbali mbali ndani ya mwaka jana.

MWISHO