Saturday, January 18

HABARI PICHA: Spika BLW aweka jiwe la msingi jengo la kituo cha Ununuzi wa Karafuu na Jengo la Huduma za Kibenki ZSTC Madungu Chake Chake Pemba

AFISA Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Ahemd Abubakar, akicheza ngoma ya Msewe kutoka Kambini Kichokochwe katika moja ya sherahe za uzinduzi wa miradi ya maendeleo Pemba, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar

 

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, akitoa maelekezo kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulidi, alipowasili katika jengo la uwekezaji ZSTC Mdungu kwa uwekaji wa jiwe la msingi, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zebeir Ali Maulid, akikunjua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi Jengo la Uwekezaji ZSTC Madungu, kushoto ni Mama Warda Zubeir na waziri wa biashara na maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulidi, akimsikiliza waziri wa biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaabban, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la uwekezaji ZSTC Madungu, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar
MKUU wa Mkoa wa KUsini Pemba Mattar Zahor Massoud, akitoa salamu za wananchi wa Mkoa huo kwa spika wa baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid, wakati wauwekaji wa jiwe la msingi jengo la uwekezaji ZSTC Madungu, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
BAADHI ya wanachama wa chama cha ACT Wazalendo, wakifuatialia uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo la uwekezaji ZSTC Madungu Chake Chake Pemba, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar
WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la uwekezaji ZSTC Madungu Chake Chake, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Chake Chake, wakati wauwekaji wa jiwe la msingi jengo la Uwekezaji ZSTC Maungu Wilaya ya Chake Chake, ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)