Thursday, January 16

VIJANA kisiwani Pemba wametakiwa kutumia fursa zilizopo ili kujiimarisha kiuchumi na kujiondoa katika wimbi la umasikini.

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais sera uratibu ya Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma akizungumza na wananchi mbali mbali wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni, ikiwa ni shamra shamra ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib akizungumza na wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni, ikiwa ni shamra shamra ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Vijana Fatma Hamad Rajab akitoa maelezo juu ya ujenzi wa Kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni,ikiwa ni shamra shamra ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais sera Uratibu wa Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni,Ikiwa ni shamra shamra shamra ya Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
FISA Mdhamini wa Wizara ya Habari Utamaduni na Vijana Mfamau Lali Mfamau akizungumza na wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni, ikiwa ni shamra shamra ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
WASANII wa Kikundi Cha JUFE wakiongozwa na “Mwinyi mpeku” akionesha onesho lao wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni, ikiwa ni shamra shamra ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
KIKUNDI Cha wasanii “Swaga” wakiimba wimbo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni,ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

WANAFUNZI was Skuli ya Sekondari Limbani na Chasasa Wete wakifuatlia Kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais, Sera na Uratibu ya Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo Cha elimu Kwa vijana huko Weni, ikiwa ni shamra shamra ya Maadhimisho ya kutimia miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

(PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)

NA ZUHURA JUMA, PEMBA

VIJANA kisiwani Pemba wametakiwa kutumia fursa zilizopo ili kujiimarisha kiuchumi na kujiondoa katika wimbi la umasikini.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Hamza Hassan Juma katika uwekaji wa jiwe la msingi kwenye kituo cha mafunzo kwa vijana huko Weni Wete Pemba, ikiwa ni katika shamra shamra za kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar,
Alisema kuwa, Serikali inajitahidi kuwawekea mazingira mazuri wananchi wake ili kuwawezesha kiuchumi, hivyo ni vyema wakazitumia fursa zilizopo kwa lengo la kukuza kipato chao, jambo ambalo litasaidia kuondokana na umasikini.
“Kituo hiki kitatoa elimu ya mambo mbali mbali ya ujasiriamali, hivyo kitakapomalizika muje mujifunze, kwani elimu hiyo itawasaidia katika kuanzisha miradi na kukuza uchumi wenu”, alisema Waziri huyo.
Mhe: Hamza alifahamisha kuwa, ujenzi wa kituo hicho ni miongoni mwa matunda ya Mapinduzi Zanzibar, hivyo kuna haja ya kuhakikisha wanapata elimu ipasavyo kwa lengo la kujikomboa.
Alisema kuwa, vijana wana vipaji vingi, ingawa ukosefu wa Elimu ndio unaosababisha kukosa fursa kadhaa za kiuchumi na kuiomba Wizara kuwaandaa vijana hao, ili waweze kuzichangamkia fursa.
“Fursa zipo nyingi na zinaendelea kumiminika, lakini ikiwa hatukuwaandaa kielimu watazikosa, kwani hata kuandika miradi hawajui, hali ambayo wakati mwengine wanakosa hata fedha za mkopo”, alisema Waziri huyo.
Akitoa taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab alisema, mradi huo umepangwa kugharimu shilingi milioni 280 mpaka kumalizika kwake, ambapo kwa sasa upo katika hatua za mwisho.
Alisema kuwa, kituo hicho kitawaanda vijana kuwa viongozi imara, wajasiriamali wazuri na kuweza kujiongezea kipato katika kazi zao za ujasiriamali.
“Lengo la Serikali ni kuwaendeleza vijana kiuchumi na ndio maana katika fedha za Uviko zilizotengwa kwa wajasiriamali, asilimia 45 zimelelekezwa kwa vijana “, alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib alieleza kuwa, nia ya Dk. Hussein Mwinyi ni kuwasogezea huduma Bora wananchi wake, ambapo ameleta miradi mbali mbali itakayowawezesha kupata ajira na kujiari wenyewe kwa lengo la kujikwamua na umasikini.
“Rais wetu anajitahidi sana kuboresha maisha yetu, hivyo tumuunge mkono kuhakikisha anafanikiwa malengo yake ambayo ndio malengo ya Mapinduzi Zanzibar “, alisema Mkuu huyo.
Kituo hicho cha mafunzo kwa vijana kinalenga kuwakomboa vijana kiuchumi, ambapo Wizara ina mpango wa kuvijenga kila Wilaya, ili kuhakikisha wanapata elimu ambayo itawasaidia kuanzisha miradi mbali mbali.
                       MWISHO.