NA AMINA AMHED, PEMBA
UONGOZI wa Shehia ya Wawi Jimbo la Wawi wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba, umesema utatoa kila aina ya ushirikiano na msaidizi wao mpya wa sheria, katika kutatua changamoto mbali mbali za jamii zikiwemo matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia, ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikikosa ufumbuzi, kwa kutokuwepo msaidizi wa sheria makini.
Hayo yalielezwa Januari 22, 2023 na Sheha wa Shehia ya Wawi Sharifa Ramadhan Abdalla, alipokuwa akifungua mkutano maalum wa kutoa Elimu kwa wajumbe wa sheha wa shehia hiyo, kutoka kwa Msaidizi moya wa sheria Kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Chake Chake Pemba ‘CHAPO’.
Alisema anaamini kuwa Idara ya Katiba na Masaada wa Kisheria kumuwezesha Msaidizi huyo wa sheria, haikukosea, kwani amemuwa mtendaji mzuri na mfuatuliaji hata kabal ya kupata mafuanzo ya awali ya sheria na sasa kuijiunga na CHAPO na kuwa katika shehi hayo.
Alisema kwa anavyomfahamu Msaidizi huyo wa sheria, naamini zile chhamgamoto mbali mbali ikiwemo kero la udhalilishaji, ambazo zinaendelea zinajitokeza katika vijiji vilivyomo ndani ya shehia hiyo, vinakwenda kupungua kwa kasi shehiani humo.
Sheha huyo alieleza kuwa, kilichobakia kwa jamii na wajumbe wa sheha ni kumpa ushirikiano wa dhati Msaidizi huyo wa sheria ili aendelee kuisaidia jamii katia majanga mbali mbali na hasa wizi, udhalilishaji na matumizi ya dawa za kulevya.
”Kwanza sisi uongozi wa shehia ya Wawi tumefarajika kwa elimu uliyotupa na tunajivunia kuwa na Msaidizi wa sheria wewe, maana kila mmoja anajua utendaji wako wa kazi na ufuatialiaji wako na sisi tutakupa ushirikiano wa hali na mali,”alieleza.
Katika hatua nyingine sheha huyo wa shehia ya Wawi, alisema kama jamii ikishirikiana kwa moyo wa kweli, hakuna ovo wala uhalifu wa wowote utakaoshinda ndani ya shehia ya Wawi.
“Uwepo huu wa Msaidizi wa sheria ndani ya shehia hii ya Wawi, itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi, katika kutatua baadhi ya kesi hasa za madai, kwani zipo ambazo huishia kienyeji ni kutokana na kukosa msaada wa kisheria katika jamii,”alisema sheha huyo.
Akizungumza katika mkutano huo Msaidizi huyo wa sheria jimbo la Wawi kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake Chake CHAPO. Haji Nassor Mohamed, alisema kuwa kwa kushirikiana na uongozi wa shehia, Msaada wa kisheria utawafikia wananchi katika maeo mbali mbali tena bila ya malipo.
Alisema kuwa, sasa yuko tayari kutumwa na wananchi wenzake, ili kutoa elimu ya kisheria, ushauri na msaada bila ya malipo, kwani ndio msingi mkuu wa upatikanaji haki kwa jamii ya jimbo la Wawi.
Msaidizi huyo wa sheria alieleza kuwa, Idara ya Katiba na Msaada wa sheria ilitumia gharama kubwa kumuwezesha, sasa hana budi kutimiza malengo ikiwa ni pamoja na kuitumikia jamii wakati woowte.
Hata hivyo ameuomba uongizi wa shehia ya Wawi na jimbo kwa ujumla kumpa ushirikiano wa hali na mali, ili kufanikiisha kuifikia jamii, katika kupata na kutetena haki zao.
”Inawezekana jamii yetu imeshakata tamaa kufuatilia haki zao katika vyombo vya sheria, sasa uwepo wangu mimi na tukishirikiana hatua kwa hatua tunaweza kufikia malengo na kuirejeshea serikali imani kwa wananchi wake,”alieleza.
Mapema mjumbe wa Bodi ya CHAPO Zuwena Hamad Ali, alisema CHAPO imepama mtu madbuti na makini kwenye utendaji wa kazi hasa wa kujitolea.
Alisema, msaidizi huyo wa sheria anamfahamu vyema utendaji wake wa kazi tokea akiwa mwandishi wa habari, sasa kilichobakia kwa wananchi wa Jimbo la Wawi ni kumtumia ili kushirikiana katika utatuzi wa changamoto mbali mbali.
”Kwanza niseme kuwa, kwa changamoto tulizonazo shehia ya Wawi na aina ya Msaidizi wa sheria tulienae kama tutashirikiana zitapungua kwa kiwango kikubwa mno,”alifafanua Mjumbe huyo wa Bodi ya CHAPO.
Nao baadhi ya washiriki wa Mkutano huo akiwemo Mjumbe wa sheha wa shehia hiyo katika kijiji cha Wawi Mtemani Nassor Rashid aliwataka wananchi wa Wawi kutodharau Viongozi wa Shehia wanapofikwa na changamoto mbali mbali na kukimbilia vyombo vikubwa kabla kupitia katika uongozi wa shehia ili kuepusha Mivutano isiyoya lazima.
Katika mkutano wajjumbe hao wa shehe wamefundishwa nini maana na ushahidi, aina za ushahidi, sababu za kutoa ushahidi, changamnoto kwa mashahidi, nani mtoto kisheria na changamoto katika kuendesha kesi za udhalilishaji kwa watoto wenye miaka katia ya 15 hadi 17 mahakamani.
Mwisho.