Saturday, January 25

Tumieni takwimu katika habari za wanyamapori ili watanzania waweze kufahamu idadi na aina za wanyama waliopo- mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa Tanzania

NA ABDI SULEIMAN.

WAANDISHI wa Habari wa uhifadhi wa wanyamapori na utalii Tanzania, wameshauriwa kutumia takwimu katika bahari za wanyamapori katika habari zao ili watanzania waweze kufahamu idadi na aina za wanyama waliopo na wanaopotea kutokana na mambo mbali mbali.

Ushauri huo umetolewa na mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa Tanzania Nuzulack Dausen, wakati aliwasilisha mada ya kwa waandishi wa habari juu ya mbinu za kuripoti habari za uhifadhi wa wanyamapori, mradi kupitia mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, unaotekelezwa na JET Tanzania kwa ufadhili wa shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID).

Alisema takwimu za wanyama zipo ni vizuri kuzitumia katika habari zao ili watanzania wataweza kujuwa idadi sahihi ya wanyama na aina ya wanyama walipo na wanaopotea kwa sababu gani.

Alifahamisha kwamba uandishi wa habari wa sasa umebadilika na sio kama ule wa miaka 50 iliyopita sasa unaenda na mabadiliko ya dunia katika kazi.

Hata hivyo aliwataka waandishi hao kuwahakikiwa wanafanya utafifi wakina katika kugundua wanambao ni adimu na wanapotea, ili kuhakikisha jamii na wananchi hawaharibu au kuvamia maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kulinda wanyama hao.

“Zipo bionuaiadimu kupatikana sehemu yoyote ile duniani, iwapo tutaendelea kuzipoteza siku hadi hadi siku, wajibu wetu waandishi kuhakikisha jamii inapatiwa elimu ya kina, ili kuepusha kuvamia maeneo ya hifadhi kwa jili kilimo na malisho,”alisema.

Kwa upande wake mkufunzi wa mabadiliko ya Tabinachi na bionuai Joseph Olila, alisema baadhi ya bionuai za viumbe vidogo vidogo kama chura na kinyonga, vipo hatarini kupotea kutokana na mabadiliko ya tabianchi yanayoikubwa tanzania.

“Viumbe hivi haviwezi kusafiri masafa marefu kutafuta mahitaji yao, mabadiliko yanapozidi baadhi ya viumbe vinaweza kupotea kwa kushindwa kuhimili mabadiliko hayo,”alisema.

Naye meneja ufuatiliaji na Tathmini USADI Tuhifadhi Maliasi John Steven Noronha, alisema watanzania 560 waliuawa na samba katika kipindi cha mwaka 1990 hadi 2004 huku 308 wakijeruhiwa.

Aidha alisema mwaka 2012/2019 watanzania 1,069 wamefariki dunia kwa kushambuliwa na wanyama, huku 204 wamepata ulemavu wa kudumu na mifugo 792 imekufa, huku hekta 41,404 zimeharibiwa na wanyamapori ndani ya kipindi hicho.

Mwandishi wa habari kutoka Tanzania Daima Janeth Jovin, amesema waandishi bado wanakazi kubwa ya kufanya ili kuwe na usimamizi mzuri wa shoroba ambazo ndizo tegemeo kubwa kwa wanyamapori.

“Iwapo shoroba zitatoweka zote basi watalii hawatokuja tena Tanzania, wamanyama watakosa maeneo yao ya malisho na mahitaji yao,”amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET), John Chikomo alisema kumekuwa na ongezeko la wanyamapori katika baadhi ya hifadhi, jambo ambalo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na uhifadhi wa wanyamapori.

“Hata ongezeko la watalii wanaoingia nchini ni mafanikio yanayotokana na elimu ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori inayotolewa mara kwa mara kwa waandishi wa habari hapa nchini,” alisema.

Hata hivyo aliwataka waandishi wa habari kuhakikisha wanakuwa makini katika kuandika habari za takwimu za wanyamapori, ili kuona wananchi wanakuwa marafiki wa wanyamapori.

Naye Mwandishi Exuperius Kachenje, alisema waandishi wanamchango mkubwa wakuelimisha jamii juu ya umuhimu wa shoroba, ili kujuwa umuhimu wa uhifadhi na kulinda hifadhi hizo.

Mwanishi wa habari kutoka TBC Swalehe Makoye, alisema jukumu la kuelimisha jamii bado litakua ni waandishi, juu ya umuhimu wa kulinda na kuhifadhi shoroba za wanyamapori nchini, kwani zina mchango mkubwa kwa jamii na wanyama.

MWISHO