Monday, January 27

TAMWA ZANZIBAR YATOKA HADHARANI KULALAMIKIA TAFSIRI YA KISHERIA WAKATI WA UTOAJI HUKUMU, KISHA YATOA MAPENDEKEZO

HAJI NASSOR, PEMBA.

HUKUMU tofauti inayotolewa na Majaji na Mahakimu hasa kwenye mahkama za kupambana na makossa ya udhalilishaji Zanzibar, yaibua hisia tifauti.

Maana wapo wanaohoji, ikiwa kila Hakimu anaendesha na kutoa hukumu kwa kufuata sheria anayoijua yeye, kinyume na zile za Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, au ile ya Mwanendo wa makossa ya jinai nambari 7 ya mwaka 2018.

Mfano mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto Aisha Hamud wa Wete, anahoji ikiwa pia Majaji na mahakimu hao, hawaitumii ile sheria ya Ushahidi nambari 9 ya mwaka 2016.

Wengine wakilalamikia uwepo wa adhabu tofauti hapa Zanzibar, kwa wakosaji na watiwaji hatiani kwa kosa la aina moja na kwa mtu mwenye umri wa utoto kisheria.

Mratibu wa TAMWA Pemba Fat-hya Mussa Said, anasema hapati jawabu kamili anpojiuliza suali, ikiwa mahakimu wa anatumia sheria moja iliyopitishwa Baraza la wawakilishi.

‘’Tulitarajia tuskie kuwa, wapo washtakiwa waliofungwa miaka 30 au kifungo cha maisha Chuo cha mafunzo, kwa kesi za ubakaji kama sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 invyoelekeza,’’anasema.

Tatu Abdalla Msellem, anasema hajaona tofauti kwa hukumu kali, kabla yam waka 2018 kuwepo na sheria mpya na ule wamaka 2004 zilipozaliwa sheria hizo, zilizofanyiwa marekebishao mwaka 2018.

‘’Maana utaskilia makossa ya udhalilishaji hayana dhamana na sasa ukitiwa hatiani, ni kifungo kisichopungua miaka 30 au chuo cha mafunzo maisha, lakini yote hayapo hayo,’’analalamikia.

Wananchi Salma Haji Kombo wa Msingini Chake chake na mwenzake Zuwena Himid Nassor wa Matale wanasema, mwaka 2018 baada ya kupitishwa sheria hizo, waliingia hamu kuona makosa hayo asa yamefikia mwisho.

‘’Tunazo sheria mpya kuanzia mwaka 2018 kama vile ile ya Ushahidi, Adhabu na ya Mwendo wa makosa ya jinai, lakini bado washtakiwa wnaafungw amiaka saba, au 20,’’wanalamika.

WAHANGA

Mama ambae mtoto wake alibakwa na mashitakiwa mwalimu wa skuli ya msingi Madungu Ali Makame Khatibu (kesi namba 36/2022) alishangaa licha ya kutiwa hatiani, lakini alifunguwa miaka 4 na fidia ya shilingi milioni1.

‘’Bado hadi leo najiuliza Hakimu yule alitumia kifungu kutoka sheria gani ambayo inampa uwezo kuacha miaka 30 au kifungo cha maisha na kumfunga miaka 14, kwa hatua hii makossa hayamalizi,’’anaeleza.

Mzazi mwengine ambae mtoto wake aligundulika kulawitiwa na mshitakiwa Fadhil Mussa Saharif, (kesi namba 53/2021) anasema kidogo, aliona mfano wa sheria ilivyofuatwa, kwa Hakimu husikua kumfungwa miaka 30.

‘Watu alishangaa na wengine wakidhani tumetoa rushwa, ili afungwe miaka mingi, lakini ndioe sheria inavyoekeleza, ingawa sio mahakimu wengi wanaofanya hivyo,’’anasema.

Aidha taarifa kutoka mahakama ya kupambana na udhalilishaji ya mkoa wa kaskazini Pemba, ipo kesi (namba 36/2022) ikihusisha kosa la kubaka, ambapo mshitakiwa Ali Hassan Hamad, baada ya kutiwa hatiani, alifungwa miaka 30 na fidia ya shilingi milioni 2.

Lakini baba wa mtoto wa miaka 9, alipatwa na mshangao, baada ya Mahakama kumfunga miaka 20 mshitakiwa Masoud Khamis Mussa, licha kutiwa hatiani na ushahidi usio na shaka.

‘’Mahakama nyingine kwa kosa kama hili mshitakiwa anafungwa miaka 30, lakini mbona huyu kafungwa miaka 20, kifungu hichi kinatokea, wapi,’’alihoji baba huyu.

WANANCHI WA KAWAIDA

Ali Khamis Juma (50) wa Wawi Chake chake anasema kasoro na mifumo iliyopo ya mahakama kama haijarekebishwa, kusjitarjiwe mabadiliko katika jamii.

Salma Omar Kassim (25) anasema kama sheria ilipotishwa kihalali na chombo rasmi, hakuna budi ituke kama ilivyo, ili kukosema matendo hayo.

Mtoto Khadija Haji Said (17) anasema wataendelea kubakwa na kulawitiwa, ikiwa mifumo na uendeshaji wa kesi mahakamani na utoaji wa hukumu hauko sawa.

‘’Utaskia mbakaji mmoja kwafungwa miaka 20, mwengine miaka 7 na mwengine anafungwa miaka 30, sasa sheria kama haikufuatwa kama ilivyo, bado tutaendelea kuumizwa,’’anasema.

WADAU

Mratibu wa Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Mashavu Juma Mabrouk, anasema kama kasoro za kisheria hazikutafiwa ufumbuzi watoto wataendelea kuathirika, ingawa kwa wenye ulemavu ni mara mbili yake.

Afisa Mawasiliano TAMWA-Pemba Gaspery Cahrles anasema, TAMWA inasikitishwa na mifumo isiyofanana katika mahakama Zanzibar.

‘’Mifumo ya hukumu na usikilizaji wa kezi za udhalilishaji bado haujakaa sawa Zanzibar na ndio maana kila hakimu ana hukumu yake, kwa washtakiwa wa makossa hayo,’’anasema.

Wakili wa kujitegemea Pemba Zahran Mohamed Yussuf, anasema bado harufu ya rushwa imekuwa ikitikisa wakati wa kuendesha na kusikiliza kesi za udhalilishaji.

Wakili wa serikali Ali Amour Makame, anase mfumo wa usikilizaji wa rufaa sio rafiki kwa waathiriwa wa kesi za Udhalilishaji.

Akisema kwa kawaida katika rufaa yanaangaliwa mapungufu ya kisheria na kimaalezo (facts), hivyo ikiwa mshitakiwa amefungwa na mahakama iliyosikiliza kesi awali (trial court).

Lakini yalifanyika makosa kwa Hakimu au Mwendesha Mashtaka katika usikilizaji wa awali wa kesi, kasoro kubwa zinaweza kuwa na faida kwa muomba rufaa na kupelekea kuachiliwa huru.

Kuhusu kutolewa kwa fidia kama sehemu ya hukumu kwa mshitakiwa, anasema bado waathirika hanufaiki na haki hiyo, ikisababishwa na wengi wanaotiwa hatiani, hawana uwezo wala vyanzo vya fedha.

NINI KIFANYIKE

Mwanasheria huyo anasema, kwanza ni kuwepo kwa mifumo ya aina moja ya utoaji hukumu kwa wakosaji wa makossa ya udhalilishaji, ili matendo yapungue.

Mtoto Saumu Issa Khamis anasema kama sheria ilishapitishwa kwa lengo la kulinda udhalilishaji, itumike kama ilivyo, ili nao wabaki salama.

Mzazi Maryma Makame Hamad anasema, makimu wanaotoa hukumu ndogo wawe na Idara maalum wanaulizwa, ili kuhakikisha kunakuwa na mfumo mmoja.

Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali, anasema la kufanyiwa ni kurekesbishwa kwa sheria, ili kuwe na mifumo inayofanana.

Hakimu wa mahkama maalum ya kupamba na makossa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba Muumini Ali Juma, anasema bado mahakama inahaki kisheria suala la utoaji hukumu.

‘’Haina maana kila aliyetiwa hatiani anaweza kufungwa miaka 30 au chuo cha mafunzo maisha, maana kisheria ipo kujitetea, kuomba nafuu na haya yanazingatiwa na ndio maana vifungo havifanani.

                                        Mwisho