Wednesday, January 15

Wakaulima wa zao la Karafuu kutokuwaficha wahalifu wanaokata mikarafuu-RC Salama.

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, amewataka wakaulima wa zao la Karafuu ndani ya Mkoa huo, kutokuwaficha wahalifu wanaokata mikarafuu badala yake kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria ili kutiwa hatiani.

Alisema mche wa mkarafuu hadi kufikia muda wa kuzaa ni miaka mitatu (3) au sita (6), hivyo muda wote mkulima anaushuhulikia ili apate kunufaika anatokea mtu na kuukata kitu ambacho kinarudisha nyuma juhudi za mkulima.

Hayo yameelezwa na afisa Mdhamini Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Pemba Ali Suleiman Abeid, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wakulima na wadau wa zao la karafuu kwa Mkoa huo, huko katika ukumbi wa Jamahuri Holi Wete.

“kumekua na vipindi tafauti tafauti vya watu kuharibu mikarafuu, ili kuepuka kuhujumua mikarafuu lazima tuwe tayari kutoa mashirikiano ya dhati kwa viongozi wetu,”alisema.

Aidha alisema sio jambo la busara na wala kupendeza katika jamii, vizuri kushirikiana kukiwa na watu wanaonesha dalili za kuhujumu mkarafuu.

Mdhamini huyo alisema Zanzibar ilikua ndio mzalishaji mkubwa wa karafuu, baada ya kupitia vipindi tafauti katika uzalishaji wa karafuu, ZSTC, serikali na wakulima wanapaswa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha mikarafuu inalindwa na kuhudumiwa ili kupata mazao makubwa zaidi.

“Tulikuwa tunazalisha zaidi ya Tania elfu 30, lakini sasa tunazalisha Tani elfu nane na kiodo, maana yake hata zile nchi ambazo zilinza kuzalisha karafuu hivi karibuni zimeshatupita,”alisema.

Hata hivyo aliwashukuru wakulima kwa mchango mkubwa kwa shirika, kwa kuzichuma karafuu vizuri na kuzitaarisha na kuziuza ZSTC, ambapo serikali na shirika inathamini mchango unaofanywa na wakulima za ZSTC.

Kaimu kamanda wa ZAECA Mkoa wa Kaskazini Pemba Nassor Hassan Nasir, aliwashuku wakulima wa karafuu kwa msimu uliopita kuonyesha umoja na mshikamano katika kuhakikisha zao hilo wanalizua ZSTC.

Kwa upande wake Shekh Omar Hamad, aliwasihi wakulima kutokufanya udanganyifu katika biashara hiyo, kwani kufanya hivyo kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo aliwataka wakulima kutenda haki muda wote anapopeleka karafuu zao ZSTC, kwa kutokuzichanganya karafuu na makonyo na ucahfu kabla ya kwenda kuziuza.

Kwa upande wao wakulima wa karafuu Mkoa wa Kaskazini Pemba, waliliomba shirika hilo msimu wa karafuu utakapofika kutoa elimu kwa wakulima mapema, juu ya upandaji wa miche ya mirafuu na hata uchumaji wake.

MWOSHO