Wednesday, January 15

Wadau wa Sekta ya Utalii Watakiwa Kuboresha Huduma Ziendani na Mazingira ya Wakati Uliopo Kukidhi Haja. – Dk.Hussein

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Wadau mbalimbali katika Sekta ya Utalii “The Z Summit” , uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 23-2-2023

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wadau kwenye sekta ya utalii kuboresha huduma ziendane na mazingira ya wakati uliopo ili kukidhi haja na mahitaji ya wageni wanaoitembelea Tanzania.

Dk. Mwinyi alieleza hayo alipofungua tamasha la utalii na biashara “The Z- Summit” huko ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa Ndege wilaya ya mjini.

Alisema sekta ya utalii Zanzibar nyenye vivuti vingi ni sekta muhimu inayochangia asilimia 30 ya pato la taifa.

Dk. Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanazibar imechukua jitihada mbalimbali kuimarisha sekta hiyo yenye lengo la kuongeza watalii kufikia 850, 000 ifikapo mwaka 2025 ambapo tayari imeimarisha miundombinu ikiwepo kutanua barabara za kisasa, kuboresha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume ambapo alieleza kwa sasa unatoa huduma za kimataifa zenye kukidhi haja ya mahitaji ya wageni chini ya uongozi wa taasisi ya kimaifaifa ya DNATA inayotoa huduma za kimataifa za viwanja vya ndege.

Alisema ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba unaotarajiwa kuifungua Pemba kiutalii ni miongoni mwa juhudi za sreikali kwenye kukuza sekta ya utalii nchini.

Alisema Zanzibar ni kituo cha wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali ya dunia kilivyopambwa na magofu yaliyohifadhi historia pamoja na mji mkongwe uliokwenye hifadhi ya UNESCO inawavutia wageni wengi kupitia fukwe angafu, ubuluu wa bahari pamoja na ukijani wa visiwa vyake vilinavyopambwa na michezo ya baharini

Alieleza milango ya serikali ikowazi kuwakaribisha wawekezaji kuekeza kwenye michezo ya baharini ikiwemo gamu za baharini na michezo ya fukwe za bahari ikiewemo volleyball.

Akizungumzia Sera ya uchumi wa bluu na utalii Dk. Mwinyi alieleza Serikali imechukua jitihada kubwa kuitekeleza sera hiyo kwa vitendo iliwa pamoja na kutilia mkaazo suala la endelevu kupitia sera yake ya “utalii kwa wote”.

Aliahidi kuwa serikali itaendelea kuwawekeza mazingira mazuri wadau wote wa utalii na kuwaomba mkutano huo uwe chachu ya kutoa firsa nyingi kwa watalii na wadau wake. Hivyo alisema ni imani kwamba mkusanyiko huo ulioshirikisha wadau mbalimbali wa sekta utatoa mafanikio mazuri katika kuikuza sekta nchini.

“Sote kwapamoja tuungane kubadilishana uzoefu, kufanyakazi pamoja tutachangia kuikuza sekta ya utalii, Tanzania

Akizungumzia suala la kutunza mazingira endelevu, Rais Dk. Mwinyi alisema utalii ni chachu ya uchafuzi wa mazingira, hivyo aliitaka jamii, wadau wa utalii pamoja na wawekezaji kwenye sekta hiyo, kutunza mazingira na viumbe vya bahari, kuepuka ujaribifu wa ikolojia, uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa hew na maji kwa kuweka mazingira na utalii endelevu.

Mapema Waziri wa Utalii na Maliasili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Muhamed Omary Mchengerwa alieleza hali ya utalii ilivyo duniani, Tanzania inakazi kubwa ya kuitangaza nchini kimataifa kupitia sekta ya utalii.

Alisema kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usjirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanalengo la kuongeza watalii wengi kutoka mataifa makubwa duniani ikiwemo bara Ulaya, Asia, Mashariki ya Mbali na Amerika

Aidha alieleza serikali pia zina nia ya kuliteka soko la utalii kutoka China ambao wanaongoza dunia kutoa watalii wengi hadi kufikia milioni moja na nusu kwa kila nchini.

Naye, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Muhammed Said alisema wakati umefika kwa Zanzibar kubadili mtazamo kupitia misimu ya utalii kuondokana na dhana msimu mdogo na mkubwa badala yake wawetayari kuutangaza utalii misimu yote iwanufaishe wao na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa ZATI ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii, Rahim Baloo alisema mkutano huo umelenga kuitambulisha dunia na kuitangaza Zanzibar kiutalii na kiutamaduni pamoja na kuwa kuwakaribisha wawekezaji zaidi. Aidha, aliipomgeza serikali awamu na nane na wizara kwa ujumla kwa kuziungamkono sekta binafsi mchango mkubwa wanaoutoa kwa uchumi wa Zanzibar.

IDARA YA MAWASILIANO – IKULU, ZANZIBAR