Wednesday, January 15

WAHIFADHI watahadharishwa kurejea ujangili wa Tembo

KAMISHNA Msaidizi wa uhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa Abel Peter,

 

NA ABDI SULEIMAN.

KAMISHNA Msaidizi wa uhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa Abel Peter, amesema kwa Sasa changamoto kubwa inayowakabili katika hifadhi hiyo, ni kurejea kwa ujangili wa tembo hali inayopelekea kutishia maisha ya wanyama hao katika hifadhi.

Alisema tayari kwa kushirikiana na wananchi, waliweza kukamata nyara 12 zinazotokana na tembo sita (6) katika Kijiji Cha Sanje na mlimbo walikamata nyara tatu zinazotokana na tembo wawili (2), matukio yote yametokea miezi miwili iliyopita nje ya hifadhi.

Kamishna msaidizi Abel, aliyaeleza hayo wakati alipokua akiwasilisha taarifa fupi ya hifadhi ya taifa milima ya Udzungwa, katika ziara ya wandishi wa habari za uhifadhi wa wanyamapori na utalii Tanzania kutoka JET, kupitia mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, huko Wilaya ya kilombero halmashauri ya mji wa Ifakara Mkoa wa Morogoro.

Alisema wanaofanya ujangili huo, wanafanya nje ya hifadhi kwani ndani ya hifadhi ulinzi umeimarishwa zaidi, na matukio hayo hutokea usiku, kwani ndio muda tembo hutoka hifadhini na kwenda kutafuta chakula nje ya hifadhi.

“Sisi taarifa za matukio haya tumepewa na wananchi, ambao wanajua thamani ya Tembo na hawapendi matukio hayo kutoka, baade tukashirikiana nao na kufanikiwa kuzikamata nyara hizo kabla ya kusafirishwa,”alisema.

Alifahamisha kwamba biashara ya ujangili haiishi na wanaohitaji wanaendelea kuhitaji bidhaa hiyo, ila kwa Sasa tumeimarisha ulinzi zaidi katika hifadhi pamoja na uraiyani, kuna vijana maalumu wanatoa taarifa za tembo kutoka hifadhini na kuanza kufuatiliwa.

Muhifadhi Abel alisema, licha ya kuwepo kwa Sheria kali na kuwatia hatiani wanaojihusisha na biashara hiyo ya ujangili, lakini mikakati zaidi inapaswa kuimarishwa na Sheria ongezewa makali kwa watakaopatikana na meno ya tembo.

Alisema kwa wanaendelea kutumia doria mbali mbali katika kuwasaka wanofanya ujangili, pamoja na kutumia mbinu za kisasa ili kuona wanadhibiti kabisa kutokuendelea kwa biashara hiyo.

Aliwataka wananchi waliozungukwa na hifadhi ya milima ya Udzungwa na hifadhi ya taifa ya Nyerere, kuendelea kushirikiana ili kuona wanyama wanapotoka hifadhini wanaweza kudishwa katika hifadhi zao.

Meneja wa Shoroba, kutoka Mpango wa kuhifadhi Tembo kusini mwa Tanzania (STEP) Joseph Mwalugelo, alisema matukio ya ujangili wa tembo yameanza kutokea, lakini juhudi za wananchi wameweza kuzikamata nyara hizo.

Alisema wananchi baada ya kujuwa umuhimu wa wanyama hao kwa taifa, wameweza kuwa msaada mkubwa katika kuwahikisha matukio ya ujangili hayatokei tena.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JET John Chikomo, aliwataka waandishi wa habari wa uhifadhi wa wanyamapori na utalii, kutumia kalamu zao kuelimisha jamii juu ya kuweka ulinzi shirikishi katika kuhakikisha wanatokomeza ujangili wa Tembo ambao tayari umeshaanza kurudi tena.

Nao wananchi waliotoa maeneo yao kwa ajili ya kuruhusu mradi wa shoroba upite, wamewataka wahusika kuhakikisha mradi huo unamalizika ili tembo kupita katika maeneo yao na kuwanusuru na matukio ya ujangili.

MWISHO

Abdi Juma Suleiman

Journalist/Photographer

Zanzibarleo newspaper
Chake Chake -Pemba
+255774565947 or +255718968355