Tuesday, January 14

HIFADHI YA TAIFA YA UDZUNGWA -Inyohifadhi miti aina 2500, wanyama aina 12 ni kivitio cha watalii

                 HIFADHI YA TAIFA YA UDZUNGWA

maji yakitoka juu ya milima inayopatikana katika hifadhi ya taifa ya Udzungwa

 

-Inyohifadhi miti aina 2500, wanyama aina 12 ni kivitio cha watalii

 -Maporomoko yake ya maji ndio chanzo cha uzalishia umeme wa Kidatu

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

Ni eneo tulivu likiwa na mazingira mazuri ya kuvutia, hali ya hewa yenye ubarid baridi ndani yake, huku sauti za wanyama mbali mbali zikisikika, ikiwemo ndege na Kima.

Sauti ya maporomoko ya maji yakisikika kwa ukaribu kutoka ndani ya maporomoko ya maji yaliyoko ndani ya hifadhi hiyo ya milima ya Udzungwa.

Hifadhi ya milima ya Udzungwa ipo katika Wilaya ya Kilombero halmashauri ya mji wa Ifakara, katika mkoa wa Morogoro ambapo kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi 2022 mkoa una watu 3,197,104 wanaume ni 1,579,869 na wanawake ni 1,617,235.

Mkoa huo, unavivutio vya utalii, ukihusisha mbuga zenye bioanuai, mandhari za kupendeza, kama vile milima, maporomoko ya maji, vyanzo vya maji, na wanyamapori, ndege wa aina mbalimbali, mapango ya kihistoria.

Mkoa huo umejaaliwa kuwa na hifadhi mbali mbali, ikiwemo msitu wa asili, hifadiu ya taifa ya mlimima ya Dzungwa, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Pori la akiba la Selous, Pori Tengefu la Kilombero na Hifadhi ya Jamii.

Hivi karibuni Timu ya waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET), Uhifadhi wa wanyamapori na utalii, walifanya ziara ya kutembelea hifadi ya Milima ya Udzungwa, Shoroba ya Kilombero na kuzungumza na wananchi waliopitiwa na Shoroba hiyo, chini ya Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili.

baadhi ya ndege wanaopatikana katika hifadhi ya taifa ya Udzungwa

HIFADHI YA MILIMA YA UDZUNGWA

Hifadhi hii inaukubwa wa kilomita za mraba 1,990, ni hifadhi yenye viumbe ambavyo, havipatikani maeneo mengine kokote duniani, ikiwemo ndenge aina ya Mbega wekundu (Iringa red colobus), Sanje crested mangabey, chozi kibawa chekundu (Rufous-winged sunbird) na Kwale kugunduliwa (Patridge-like Francolin) na kware wa udzungwa.

Maporomoko ya mto Sanje yenye urefu wa mita 170 yakianguka na kutua mithili ya ukungu, aina ya maua adimu (African violet), vyote vinapatikana ndani ya hifadhi hiyo.

Kamishna Msaidizi wa uhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa Muhifadhi Abel Peter, anasema hifadhi iko katika tawi la Mashariki katika maeneo yenye viumbe hai, kuna aina 12 za wanyama primate na kati ya hizo aina mbili, ndio zinazopatikana udzungwa.

Anasema kuna aina tisa (9) za misitu ya asili, na ndio hifadhii ya pekee yenye eneo kubwa, muna aina 2,500 za miti, inayopatikana udzungwa pekee.

Hifadhi hiyo inazalisha zaidi ya mito 31 ndio eneo lenye chanzo kikubwa cha maji kutoka katika maporomoko ya Udzungwa.

Udzungwa ndio chanzo kikubwa cha maji kinachopeleka katika bwawa la Kidatu, kwenye chanzo cha umeme, bwawa la kianzi, maji mengine hutumika katika shughuli za kilimo.

Kamishna msaidizi Abel, anasema eneo la Udzungwa ni eneo muhimu la kulinda na kuhifadhi maji, pia ni vyanzo vya mito, inayopeleka maji mto mkuu wa Ruaha, Kilombero na Rufiji, ambayo hutumika kwa shughuli za kijamii ikiwemo kilimo na uvuvi.

“Mwaka mzima mito inatiririsha maji, neo linahitaji matunzo na usimamizi madhubuti, ili iweze kutiririsha maji kila uchao, hapa mazingira yake ni ubaridi muda wote na wageni wanavutia na maumbile ya asili yanayopatikana humu,” anasema.

SHUGHULI ZA KIUTALII

Msaidizi Abel anasema, kikubwa kinachofanyika mbali ya uhifadhi, pia shughuli za kiutalii kwani kuna njia za kiasili za kutembelea, watalii kungia katika hifadhi, na kwenda kwenye maporomoko ya maji SANJE.

Kuna njia ya kilomita 19 ya kwenda katika kilele cha Mwaniana kwenye chanzo cha maporomoko, pamoja na njia ya kuzunguka kilomita 65, mtu anaweza kufanya utalii ndani ya hifadhi.

KAMISHNA Msaidizi wa Uhifadhi kutoka hifadhi ya Taifa ya Udzungwa Muhifadhi Abel Peter, akiwasilisha taarifa ya Hifadhi ya milima ya Udzungwa, kwa waandishi wa habari wa uhifadhi wa wanyamapori na utalii kutoka JET, kupitia mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, wakati walipotembela hifadhi hiyo katika ziara yao ya siku nne.

Aidha kwa mwaka anaesema wanapokea wageni 8,000, ambapo ni sawa na kila wageni 100, 80 ni watalii wa ndani na 20 ni wageni kutoka nje ya nchi.

Udzungwa ni hifadhi inayopendwa kwa utalii wa ndani, inatokana na namna wanavyoitangaaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari vya kitaifa.

“Tuna mipango kadhaa ya kuimarisha utalii, ni hifadhi ambayo bado haijaweza kujiendesha kiwango cha pesa wanachozalisha kwa mwaka, haziwezi kuendesha shuhuli za uhifadhi,” amesema.

Anasema mwaka wanazalisha shilingi milioni 250 hadi shilingi milioni 300 na fedha wanayotumia, kuendesha hifadhi ni karibu shilingi 1.2, bado ni hifadhi tegemezi na wapo nyuma uzalishaji.

UPANDE WA WANYAMA

Hifadhi ina aina 12 ya wanyama pori, wakiwemo Nyati, Simba, Chui, Nyumbu, Ngiri, Punda milia, Tembo, Swala na Twiga huku Faru akikosekana.

Aidha anasema kwa sasa changamoto kubwa wanayoikabili ni kurejea kwa ujangili wa tembo, hali inayopelekea kutishia maisha ya wanyama hao katika hifadhi hiyo.

“Tayari kwa kushirikiana na wananchi, tuliweza kukamata nyara 12 zinazotokana na tembo sita (6) katika kijiji cha Sanje na mlimbo, walikamata nyara tatu zinazotokana na tembo wawili (2), matukio yote yametokea miezi miwili iliyopita nje ya hifadhi,”amesema.

“Sisi taarifa za matukio haya tumepewa na wananchi, ambao wanajua thamani ya Tembo na hawapendi matukio hayo kutoka, baade tukashirikiana nao na kufanikiwa kuzikamata nyara hizo kabla ya kusafirishwa,”amesema.

Aidha amesema biashara ya ujangili haiishi na wanaohitaji wanaendelea kuhitaji bidhaa hiyo, ila kwa Sasa tumeimarisha ulinzi zaidi katika hifadhi pamoja na uraiyani, kuna vijana maalumu wanatoa taarifa za tembo kutoka hifadhini na kuanza kufuatiliwa.

MSITU WA MAGOMBELA.

Ni msitu wa asili ambao umehifadhiwa, ni eneo lenye baadhi ya viumbe adimu vinavyopatikana humo, ikiwemo mbega wekundu, ni eneo ambalo watu wanataka wafeke na kulima mpunga, pamoja ba bioanuai adimu na walioko hatarini ya kutoweka.

WAANDISHI wa habari wa uhifadhi wa wanyamapori na utalii kutoka JET, kupitia mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, wakipanda ngazi mara baada ya kurudi kuangalia maji yanayomwagika katika moja ya vyanzo vya maji vinavyopatikana ndani ya Hifadhi ya Udzungwa.

WANANCHI WALIOZUNGUKWA NA HIFADHI HIYO

Juma Mahula kutoka kitongoji cha Melisa, anasema hifadhi hiyo imekua ni moja muhimu kwao, kwani wageni mbali mbali wamekuwa wakitembelea na kupata kununuliwa kwa biashara zao.

“Sisi wengi hapa ni wakulima na wafanya biashara ndogo ndogo, tumekua tukinufaika na hifadhi hii, kwa baishara zetu kununuliwa siku zinakwenda,”amesema.

Naye Isaya Utambule anafahamisha kwamba, maji yanayotoka katika hifadhi yamekua yakimwaga maji ndani ya mashamba yao, hali inayopelekea kunawirika kwa mazao wanayolima.

“Hapa unachipanda kinaota tena kinanawiri vizuri, hii nikutanona na ardhi bado haijatiwa kemikali hafalu na maji muda wote yapo,”amesema.

Afisa mtendaji kata ya Mangula Bright Aldo Mwinyi, anasema hifadhi imakuwa na faida kubwa, kwani baadhi ya wananchi wamepata pesa kutokana na kulipwa fidia kufuatia kutoa ardhi yao kupisha mradi wa ushoroba.

WAANDISHI WA HABARI

WAANDISHI wa Habari wa Uhifadhi wa wanuamapori na utalii kutoka JET, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea moja ya maeneo ambayo maji yanamwagika kutoka katika maporomoko ya maji yanayopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Udzungwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa ‘JET’ John Chikomo, amesema waandishi wa habari wameweza kujionena hifadhi hiyo na umuhimu wake kwa jamii.

Anasema waandishi wa habari watakua mabalozi wazuri kwa kuindikia na kuitangaza hifadhi hiyo, pamoja na matunda yaliyopatikana kwa wananchi juu ya kuwepo kwa ushoroba.

“Kwa sasa sisi JET tupo katika utekelezaji wa mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, mradi huu umekua ukitoa mafunzo kwa waandishi na ziara, sasa suala la uhifadhi litaenda kufanyiwa kazi ili jamii isiharibu hifadhi, kwnai hifadhi inategemea jamii na jamii inategemea hifadhi.

MABADILIKO YA TABIANCHI HALI IKOJE?

Akiwasilisha mada mabadiliko ya Tabinachi na bionuai Joseph Olila, kutoka USAID Tuhifadhi Maliasili, amesema mabadiliko hayo yanapelekea baadhi ya bionuai za viumbe vidogo vidogo, kama chura na kinyonga vipo hatarini kupotea kutokana na mabadiliko ya tabianchi yanayoikubwa Tanzania.

“Viumbe hivi haviwezi kusafiri masafa marefu kutafuta mahitaji yao, mabadiliko yanapozidi baadhi ya viumbe vinaweza kupotea kwa kushindwa kuhimili mabadiliko hayo,”amefahamisha.

Aidha kupotea kwa bionuai hizo, zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa taifa, hivi sasa sekta ya utalii imekua na mchango mkubwa katika kuchangia pato la taifa kupotea kwake ni hasara kwa nchi.

Naye Afisa misitu mkuu na kiungo wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania Dk. Freddy Manyika, amesema miongoni mwa athari za mabadiliko Tabianchi ni ukame wa muda mrefu.

Jingine ni, matukio ya moto, kubadilika kwa miongo ya mvua, lakini hifadhi hii bado imeendelea kuwa katima mazingira mazuri ya haiba yake.

                   MWISHO

Abdi Juma Suleiman

Journalist/Photographer

Zanzibarleo newspaper
Chake Chake -Pemba
+255774565947 or +255718968355
MAJI yakimwagika kutoka katika maporomoko maalumu yanayopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, iliyopo katika Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mkoani Morogoro.