Friday, November 15

KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR AWAAGIZA TRAFFIC KUSIMAMIA USALAMA WA WATOTO BARABARANI

NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amewaagiza Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani kuongeza ulinzi wa watoto wakati wanapokwenda na kurudi shule ili kuepusha ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa watoto.

Akisikiliza kero za wananchi wa Shehia za Fuoni Uwandani, Migombani, Kipungani, Kibondeni, Chunga na Mambosasa Wilaya ya Magharibi B huko Skuli ya Fuoni amesema elimu inahitajika kwa Askari, madereva, abiria na watumiaji wengine wa barabara juu ya matumizi sahihi ya barabara na alama za usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi wa Polisi Richard Tadei Mchomvu amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi tayari limeshaweka mikakati ya kupunguza ajali za barabarani kwa mwaka huu 2023.

Mapema wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Aboud Jumbe Mwinyi wamesema wako hatarini kutokana na madereva kutokutii sheria za usalama barabani katika shule zilizopo karibu na barabara na kukosekana kwa Askari wakati Wanafunzi wanapoingia na kutoka Shuleni.


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1731646087): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48