NA ABDI SULEIMAN.
KIKUNDI cha ushirika cha Tumeamua kinacho jishuhulisha na ushonaji wa mashuka, kimesema kwa sasa kimeanza kupoteza mweleko baada ya mashuka 20 yenye thamani ya shilingi Milioni 1.1 (1,100,000/=) kubakia ndani baada ya kukosa soko.
Kikundi hicho kimesema kwa sasa mashuka yao yamelazimika kubakia ndani, baada ya kukosa soko la uhakika kufuatia kuwepo kwa mashuka kutoka Viwandani, ambayo bei yake hufika 10000 au 15000 na hutembezwa hadi mitaani.
Hayo yameelezwa na viongozi wa kikundi hicho, huko msuka masharibi Wilaya ya Micheweni, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ndani ya ushirika wao.
Mshika fedha wa kikundi hicho Maryam Mikidadi Omar, alisema shuka moja wanauza shilingi elfu 5,5000, tayari mashuka 20 yapo ndani kwa kukosa wateja.
“sisi hapa angalau kinachotusaidia pakitokea harusi mtu huko kama mashuka mawili au matatu, tena hukopeshwa kwa shilingi 60,000/= kwa shuka moja na kulipa kidogo kidogo, ndio tunapata kuzunguruka,”alisema.
Aidha alisema biashara hiyo kushuka imetokana na mashuka ya kisasa, kutoka viwandani yanayopitisha hadi vijijini, huku baadhi ya wafanyabiashara hukopesha pia, jambo ambalo limeua kabisa biashara hii.
Naye katibu wakikundi hicho Salma Juma Abass, alisema kukoseka kwa soko wameanza kuingia hasara, mashuka ni mengi na soko hakuna huku vijana wanaowafundisha wakiendelea kushona mengine.
Alisema changamoto kubwa kwa sasa ni ubovu wa vyarahani mara kwa mara, huku wakiangalia wanafunzi 15 wanaendelea kujifunza ushonaji wa mashuka.
Aidha alisema tayari wameshaomba mikopo katika taasisi mbali mbali ikiwemo CRDB, Wizara ya Uwezeshaji lakini hakuna taasisi iliyowapatia msaada hata mmoja.
Kwa upande wake mwanachama wa kikundi hicho Hadija Khamis Salim, alisema kabla ya kuanza kushona mashuka walikua wakifuma mafagio ambao jumala ya Mafagio ambapo fagio moja wakiuza shilingi 300, kila mtu kwa wiki mafagio matano hutakiwa kuwasilisha.
Naye bimkubwa Ali Bakari aliyomba serikali kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kuwasaidia vifaa mbali mbali, ikiwemo vyarahani, majora ya vitambaa, pamoja na kuwatafutia masoko ya kuuza mashuka yao.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, aliwataka wanakikundi hao kuwa wastahamilivu kwani serikali imekua ikishaidia vikundi mbali mbali awamu kwa awamu.
Alisema kikundi hicho kimekua mmoja ya vikundi vya mfano katika utengenezaji wa mashuka, tayari ameshawasiliana na watendaji wa Idara ya Uwezeshaji ili kuwasaidia au kuwapatia mikopo.
MWISHO