Sunday, December 29

MELI YA KIMATAIFA KUTOKA AUSTRALIA YATIA NANGA HIFADHI YA URITHI WA UTAMADUNI WA DUNIA MAGOFU YA KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyampori Tanzania (TAWA), leo  Machi 7, 2023 imepokea meli ya kimataifa ya utalii iitwayo Coral Geographer kutoka nchini Australia.   Meli hiyo yenye hadhi ya nyota tano imebeba watalii 120, ambao wametembelea Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara na kufanya utalii wa malikale pamoja na utalii wa fukwe.